Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, imewataka wanachama wenye mapenzi
mema na klabu yao kusikiliza habari kutoka ndani ya uongozi na sio zinazotoka
kwa wanaopenda kuzalisha migogoro klabuni kwao.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kulia akiwa na Msemaji wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto katika matukio ya klabu hiyo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga,
Baraka Kizuguto, alisema kwamba mengi yanayoibuliwa na watu hao yanatokana na
kuwa na malengo ya kuivuruga klabu yao.
Alisema kwamba baadhi ya watu hao wamekuwa wakiibua hoja
nyepesi, ikiwamo ya mkutano wa dharula kwa ajili ya kuleta matatizo klabuni
kwao, hivyo kila anayeipenda klabu hiyo anapaswa kusikiliza habari kutoka ndani
ya uongozi wao na si zile zinatolewa kienyeji.
“Yote yanayofanywa ni kwa ajili ya klabu ya Yanga, hivyo
nadhani kila mwenye mapenzi mema na timu hii anapaswa kuwa makini na kusikiliza
maneno kutoka kwenye uongozi, ikiwamo hatua ya kujiorodhesha kwa wale
wasioafiki uamuzi wa Juni Mosi mwaka huu.
“Watu hao hawana mapenzi mema na Yanga, ndio maana wanaweza
pia kugomea hatua ya kuorodhesha majina, ukizingatia wanachotaka wao ni kuona
klabu yetu inashindwa kuweka mipango ya kimaendeleo,” alisema.
Hatua ya kuanza kuorodhesha majina ya wanachama
wasioridhishwa na kuongeza muda wa Uchaguzi Mkuu, imetangazwa juzi na
mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, huku ikianza leo na kufikia tamati Jumamosi.
No comments:
Post a Comment