Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea
taarifa za kutolewa
wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya
mapato.
wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya
mapato.
"Tunataka ieleweke wazi kwa umma wa
Watanzania kuwa si nia yetu
kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke
kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji
mpirani.
kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke
kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji
mpirani.
"Katika mpira wa miguu wanaingia
maelfu ya watu katika kipindi kifupi. Kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda usalama
wa watazamaji na miundombinu ya viwanja ndio maana tulisitisha matumizi ya
tiketi za elektroniki hadi tujihakikishie usalama wa matumizi yake," alisema.
Tunafanya jitihada kwa karibu na mzabuni benki ya CRDB ili
kuhakikisha mfumo huu unaanza kutumika mara moja.
Kwa niaba ya sekta ya michezo
tunatoa wito kwa Serikali kushusha au kuondoa kodi kubwa zinazotozwa kwenye
vifaa vya michezo, hasa vinavyotumiwa na watoto kuanzia umri wa miaka 6-12, ili
watoto wetu waweze kuvipata kirahisi toka kwa wazazi wao ili waweze kujifunza
kucheza michezo kisasa tangu wakiwa wadogo.
No comments:
Post a Comment