Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MFANYABIASHARA kutoka Kampuni ya BinSlum Tires, Nassor
BinSlum, ameingia mkataba wa kudhamini klabu ya Stand United yenye maskani yake
Shinyanga wa mwaka mmoja.
Nassor BinSlum akikabidhi jezi itakayotumiwa na timu ya Stand United ya Shinyanga katika Ligi ya Tanzania Bara msimu ujao wa Ligi baada ya kupanda daraja, huku kampuni yake ikiwadhamini kwa mwaka mmoja.
Stand United watavuna kiasi cha Sh Milioni 50 kwa mwaka, huku
wakiahidiwa kuongezwa fedha nyingine pindi watakapoonyesha kiwango kizuri msimu
huu.
Akizungumzia leo mchana wakati wa kuingia mkataba na klabu
hiyo, mbele ya mlezi wao Steven Masele, ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga
Mjini,
BinSlum pichani.
BinSlum alisema lengo lake ni kuisaidia klabu hiyo ili ifikie malengo
yake.
Alisema ingawa fedha hizo zinaonekana kama kidogo, lakini
timu hiyo ikionyesha soka la kuvutia, basi watavuna udhamini mwingine mnono
hata kwa wafanyabiashara weengine.
“Tunataka kuona kuwa timu zetu kwa pamoja zinapiga hatua
kubwa kupata wadhamini wengine, hivyo kampuni yangu itahakikisha kuwa inafanya
juhudi kukuza soka la Tanzania.
"Stand United ifanye bidii kubwa kuonyesha kuwa wanaweza
kucheza soka, nikiamini kuwa hali hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa soka la
Tanzania,” alisema.
Naye mlezi wa klabu hiyo, Masele alimshukuru BinSlum kwa
uamuzi wake mzuri wa kuidhamini klabu yao, wakiamini kuwa mwendo huo utakuwa na
manufaa makubwa kwa upande wao.
Katika hatua nyingine, Masele aliwaambia waandishi wa habari
kuwa amejitolea kuwanunulia basi dogo la kusafiria timu hiyo iliyozaliwa Stendi
mjini Shinyanga.
No comments:
Post a Comment