KIKOSI cha
Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya
Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu
jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha
Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji
wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor
Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma,
Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin
Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
No comments:
Post a Comment