Na Cyprian Musiba, Mwanachama Yanga
WANACHAMA wa
Yanga walifanya mkutano mkuu maalumu wa klabu hiyo kujadili ajenda moja tu
kupitisha Kamati ya Maadili kama ilivyoagizwa na FIFA kupitia TFF.
Cyprian Musiba, mwandishi wa makala haya.
Lakini cha
ajabu ikaibuka ajenda nyingine kinyemela baada ya Kamati nzima ya Yanga
kutishia kutogombea tena katika uchaguzi ujao. Kukawa na
ajenda ya uongozi wa Yanga kuomba kuongezewa mwaka zaidi. Uongozi
huo chini ya mwenyekiti Yusuf Manji unamaliza muda wake mwezi wa 7 mwaka huu kwa
mujibu wa Katiba ya Yanga.
Ninachojua
mimi kama Yanga wanataka kuahirisha uchaguzi huo, walipaswa kubadili kwanza Katiba
halafu ndio wamwombe Manji aendee kuongoza. Nje ya
hapo Manji atakuwa ameichezea Katiba ambayo ndiyo iliyomweka hapo. Vinginevyo
anataka kuongoza Yanga kidikteta, kwa maana hiyo Manji hana mamlaka ya
kujiongezea muda kwa matakwa yanga. Kwa maagizo ya TFF Yanga ilipaswa kujadili
ajenda moja tu.
Manji
akafanya usanii kama kawaida yake kuwahadaa baadhi ya wanachama ili wampigie
magoti aendelee kuongoza na kutangaza kumleta Marcio Maximo na mambo
mengi ya usanii. Wanachama
wa Yanga lazima wajitambue na wajue kwamba Yanga ndio maarufu siyo na nje ya Yanga
Manji siyo Maarufu.
Yanga
inaweza kujiendesha bila Manji kwa tayari inawadhamini lukuki wa kulipa
mishahara na bado yapo makampuni makubwa na matajiri wakubwa wanaitamani Yanga
kama Qugis, Reginald Mengi, Mustafa Sabodo na wengine wengi.
Manji
asitumie udhaifu wa baadhi ya wanachama wa Yanga kutojitambua kugeuza Yanga
kama mali yake. Yanga ni mali
ya wananchi siyo mali binafsi ya Manji. Manji
anapaswa kujua kwamba siyo wanachama wote hatujitambui, karibu asilimia 97 ya
wanachama wa Yanga tunajitambua. Wanachama
asilimia 3 waliozaliwa kabla ya kuzaliwa Tanzania ndio hawajitambui na kukubali
hata kudanganywa kweupe wakati wa jua kali. Manji
anafanya biashara zake na kubwa anaangalia maslahi yake kwanza.
Manji ni
mjanja akitambua kuwa ameshamaliza kiakili wajumbe waliohudhuria aliwaletea mwanachama
mzungu ili mawazo ya wanachama ambao alikwisha kuwatengeza na kuwaandaa yabaki
wasifikiri zaidi ya hapo. Naomba
viongozi wa TFF kuisaidia Yanga ili Manji asiifanye mali yake na uchaguzi
ufanyike kama ulivyopangwa Julai mwaka huu.
Manji
anafanya kazi ya kugombana na Azam ambaye amefanya mapinduzi makubwa ya soka la
Tanzania. Manji ameshikilia media za Yanga na mkataba wake wa kushikilia media
hizo umeisha, ameshindwa hata kujenga timu bora, Manji ameshindwa kuendeleza
jengo la Mafia. Kuna wakati Manji alisema anaidai Yanga mabilioni na kushikilia
akaunti ya klabu hiyo.
Sijui kama
aliishajilipa fedha hiyo ama hajamaliza kujilipa ndio maana anaomba mwaka zaidi
ili amalizie kujilipa deni lake. Nawaomba Yanga wote tunaojitambua kupigania Yanga
ili huyu mjanja asijimilikishe. Manji
kamwe hana la maana analoweza kufanya Yanga na amekuwa na mawazo ya kuifunga Simba
tu mawazo mgando yasiyo na tija.
Mwisho naliona
yanayoendelea Simba kwa vurugu zile zinakuja Yanga kwani Kamati ya Uchaguzi ya
Yanga inaonekana wazi inafanya kazi zake kwa maelekezo na kwa maana hiyo haki ndani
ya Yanga itakuwa historia.
TFF
iokoeni na kuisaidia Yanga inakoelekea ni kubaya na vurugu kubwa zinaweza
kutokea Yanga.
Imeandikwa
na Cprian Majura Musiba.
No comments:
Post a Comment