Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), limeusimamisha
Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Simba, hadi hapo watakapofanikiwa kuunda kwa Kamati
ya Maadili itakayokuwa na jukumu la kusikiliza malalamiko yote yanayohusiana na
wagombea wao.
Kusimamishwa huko kumekuja siku chache baada ya mchakato wa
uchaguzi wa Simba kuanza, ambapo Kamati ya Uchaguzi ya Simba, chini ya Damas
Ndumbaro ilimuengua Michael Wambura kuwania Urais wa klabu hiyo, kabla ya Kamati
ya Rufaa kumrudisha kwa madai kuwa uovu upo kwa Simba, si Wambura.
Akizungumzia hilo leo mchana, jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho
hilo, Jamal Malinzi, alisema kuwa Simba inapaswa kuunda Kamati ya Maadili kabla
ya Juni 30 ili kusikiliza mashauri yatakayoletwa mbele yake na kuyatolea
ufafanuzi, jambo ambalo huenda likapokewa kwa shingo upande wa wadau wa soka Tanzania, maana klabu hiyo imetumia gharama hususan wale waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
No comments:
Post a Comment