Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu
cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo
vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya
ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130
vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Pamoja
na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za
pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu
na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
Dokta
Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak
amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi
hiki kigumu cha majonzi.
Aidha
Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze
kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku. Katika
hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe
Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi. Mheshimiwa
Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya
shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
No comments:
Post a Comment