https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Tuesday, November 17, 2015

Nay wa Mitego anaposema Mwanamke hateswi, mwanamke hapigwi, anatulizwa kwa mapenzi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Nguvu ya sanaa ni pale inapotumika kuijenga jamii bora. Tumeishuhudia sanaa mara kadhaa ikitumika kujenga misingi ya kijamii hali inayopelekea kuweka uhusiano bora na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Mtu anapofanya kazi kwa muda mrefu, anapaswa kutuliza akili yake kwa kusikiliza kazi za aina mbalimbali za kisanii kulingana na matakwa yake na mahitaji yake kwa ujumla. Unapoburudishwa na sanaa, kwa kiasi kikubwa unatuliza akili yako katika kuwaza mambo yenye tija katika mpangilio wako wa kimaisha. Katika kusikiliza sanaa, hususan ya nyimbo za kimapenzi ndio kabisa. Raha tupu. Unavuta hisia na kuondoa upweke na uchovu uliokuwa nao awali.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nay wa Mitego pichani.
Kama ilivyokuwa kwa watu wengine, msanii Nay wa Mitego ni miongoni mwa vijana waliowahi kuishi maisha magumu mno. Wakitafutwa wasanii 10 walioishi maisha magumu, kama Nay hajashika namba moja, basi hawezi kucheza namba tano kushuka. Hata hivyo kujituma, kumuomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii kumemfanya leo hii Nay awe miongoni mwa wasanii wa kiume wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva. Katika wimbo wake wa 'Mwanamke Hapigwi', Nay anadhihirisha jinsi anavyoweza kutuliza akili yake kutunga wimbo unaofundisha jamii. Ni wale wanaume wanaotesa na kuwapiga wanawake. Nay anachukizwa na hilo. Anakemea. Anasema kama umemchoka binti wa watu basi mrudishe kwao badala ya kumnyanyasa kila uchao. Katika wimbo huu niupendao sana, nakufa sana na shairi hili, 
@Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
@Acha nimbembeleze kipenzi changu wee
@Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
@Acha nimbembeleze kipenzi changu wee

Kiitikio

Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake. Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake.
Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiiiiii) Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiii).
Huwa nakosa raha, usiku na mchana bwanaaa. Napoona, dada zangu mnapigwa inaniuma. Huwa nakosa raha, usiku na mchana we bwanaa, napoona mama zangu mnateswa inaniuma.
Hata kwenye vitabu vya dini imeandikwa mwanamke ni dhaifu sana, mnapompiga na kumdhalilisha sio siri unakosea bwana
Hata kwenye vya dini imeandikwa mwanamke ni dhaifu sana, unapompiga na kumdhalilisha sio siri unakosea bwana.
Iweje umdhalilishee, iweje leo umnyanyase
Iweje umdhalilishe, iweje leo umnyanyase
Ewe mwanaume wa leo, iweje umpige mkeo, kama umemchoka mwana mwenzio basi mrudishe kwao
Ewe mwanaume wa leo, iweje umpige mkeo, kama umemchoka mwana mwenzio, basi mrudishe kwao.

Iweje umdhalilishee, iweje leo umnyanyase
Iweje umdhalilishe, iweje leo umnyanyase

Kiitikio

Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake. Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake.
Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiiiiii) Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiii).

Vesiii

Mkalime wote, mimba uikatae, mna visa bwana  wee
Hutaki kulea, unataka akatoe, ulaniwe bwana wee
Hatarisha maisha yakeee, unazipoteza ndoto zakee
Hatarisha maisha yakeee, unazipoteza ndoto zakeee
Ona anapata shida peke yake na mimba yake
Tizama katengwa ndugu jamaa zake pia na bwana ake
Onaa anapata shida peke yake na mimba yake
Tizama katengwa ndugu jamaa zake pia na bwana ake
Mlaniwe laana ziwafikie mnaopiga wanawake
Mlaniwe laana ziwafikie mnaotesa wanawake
Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
Acha nimbembeleze kipenzi changu wee
Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
Acha nimbembeleze kipenzi changu wee

Kiitikio

Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake. Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake.
Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiiiiii) Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiii).

Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
Acha nimbembeleze kipenzi changu wee
Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
Acha nimbembeleze kipenzi changu wee

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...