https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, November 04, 2015

Rais Kikwete aifanya kesho iwe sikukuu kwa ajili ya kumkabidhi IKULU rasmi Dr John Pombe Magufuli

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...