Na Mwandishi Wetu, Iringa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya Mkurungenzi wa Manispaa hii pamoja na mbunge wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa. Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa ccm wilaya ya Iringa mjini, Elisha Mwampashe alisema kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya Mkurungenzi wa Manispaa hii pamoja na mbunge wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa. Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa ccm wilaya ya Iringa mjini, Elisha Mwampashe alisema kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.
“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya 2015 haijafutwa,”alisema Mwampashe. Mwampashe ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa kuaona taarifa zinazendelea kuenena mitaani.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa, wakisikiliza hoja za aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa Mjini, Fredrick Mwakalebela na Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Elisha Mwampashe, hawapo pichani.
“Ifahamike kuwa mahakamani kuna shauri la msingi ambalo lilikuwa na kupinga matokeo na kuna shauri dogo namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya hivyo,” alisema.
Mwampashe amemalizia kwa kuwataka wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kuwa na subra kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakamani. Kwa upande wake Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo, aliesema kuwa shauri lililofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.
“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na Mkurugezi wa Manispaa ya Iringa pamoja na mchungaji Msigwa,” alisema. Mwakalebela amemalizia kwa kusema kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye pamoja na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama ndio kilichompa nafasi ya kugombea ndio maana kila kitu anachokifanya chma lazima kijue juu ya kesi hivyo.
Hii ni kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake kwa gharama hiyohiyo. Hivyo uvumi uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado haijapangwa wala kuanza kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment