https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Friday, November 27, 2015

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea na shughuli za kuijenga CCM

Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Katibu Wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa Halmashauri Kuu Oganaizesheni Ndg Mohamed Seif Hatibu katika ofisi yake Makao Makuu ya CCM, ofisi ndogo ya Lumumba jijini Dar es salaam, jana 26th Nov 2015.
Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwanasheria wa CCM Ndg Godwin Kunambi nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam, jana Novemba 26, 2015.
Mlemavu wa Viungo Ndugu Elias Ismail Mollel kutoka Arusha akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akitoka ofisini kwake, Makao Makuu ya CCM, Lumumba - Dar es salaam jioni ya jana.
Mwenyekiti wa CCM na Rais Msataafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mlemavu wa miguu Ndg Mashishanga Masanja kutoka Nzega alipokuwa akitoka ofisini kwake Lumumba Jijini Dar es salaam.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizngumza na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kimnyaki Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha alipofika kumtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya CCM, ofisi ndogo za Lumumba Jijini Dar es salaam jana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...