https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, November 16, 2015

DC wa Kinondoni Paulo Makonda awafunda waoka keki nchini Tanzania


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa tatu kulia) na Mdau wa Keki, Mama Cynthia Henjewele (wa pili kushoto), wakikata keki maalumu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Watengeneza keki Tanzania (TCBA), uliofanyika katika Mgahawa wa City Lounge Posta mpya Dar es Salaam jana. Kulia ni Mshehereshaji, Makena na Mdau wa Keki, Philip Mbonde.


Na Rahel Pallangyo, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewataka waokaji keki kufanya kazi yao kwa kushirikiana kwani inasaidia kuinua uchumi wa nchi. Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua Chama cha Waokaji keki Tanzania (TCBA) katika hafla iliyofanyika ukumbi wa City Lounge Posta mpya ambapo alikuwa mgeni rasmi.

 DC Makonda akitoa hutuba ya uzinduzi.

 Mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza (kushoto), akimlisha keki mgeni rasmi DC Makonda. Katikati ni mdau wa Keki Cynthia Henjewele.

Muakaji  keki,  Roselins Sia Adhero (kulia), akimkabidhi keki DC Makonda.
Uongozi wa TCBA wakiwa kwenye picha ya pamoja
Waokaji keki wakifurahia jambo











"Kazi mnayoifanya inalisaidia taifa kuinua uchumi kwani inatoa ajira kwa wengine kikubwa endeleeni kuwa wabunifu zaidi wa kutengeneza keki za aina mbalimbali" alisema Makonda.
Makonda aliwataka waokaji keki hao kila mmoja wao kujisogeza zaidi kwa kupanua wigo wa kazi zao kwa kuwa na vyombo vya muziki, kupiga picha za manato na video badala ya kila kazi kufanywa na mtu mwingine.
Pia aliwaambia wajiandae kwani ofisi yake imeandaa Sh.20,000,000 kwa ajili ya kushindanisha wazo bora la andiko la biashara na kuwataka nao waingie kujaribu bahati yao.
Mwanzilishi wa umoja huo, Stellah Rwabutaza alisema amesaidia kuwaunganisha waokaji keki nchini na wameweza kutambuana na kubadilishana ujuzi.
"Kwakweli umoja huu umetuunganisha sisi waokaji wa keki jambo litakalosaidia kufanya kazi zetu kwa pamoja" alisema Stellah.
Stellah alisema changamoto kubwa waliyonayo ni kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwakamata mara kwa mara ambapo waliomba watoe maelekezo ya nini wafanye ili kuendeleza kazi yao hiyo.
Naye Mwenyekiti wa TCBA,  Philip Mbonde, alisema umoja huo umewafanya wawe na mtandao wa kutafuta masoko ya keki na kujifunza ubunifu wa kutengeneza keki za aina mbalimbali.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...