https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, December 30, 2015

Viongozi wapya wa TAHLISO wala kiapo kulitumikia Shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu

Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI jana Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania


Uongozi mpya wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti  mpya wa TAHLISO  Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo  jijini Dar es salaam
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu, ukosefu wa mokopo kwa wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma, ambapo amesema uongozi wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti huyo amesema kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa serikali ya awamu ya tano.
Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa.

Viongozi wa TAHLISO wameapishwa leo rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi wa Kidemocrasia uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa katiba yao.
JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo akiapa.

Omary Idd  Naibu muazini akiapa tayari kulitumikia shirikisho hilo

Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini

Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo

Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO leo Jijini Dar es salaam
 Na Exaud Mtei (msaka habari) wa Habari24 blog

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...