https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, December 11, 2015

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akutana na mabalozi wa Norway na Malawi

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...