Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa
Kilimanjaro, Mh Amos Makalla, amewapongeza wakazi na wananchi wake katika mkoa
huo kwa kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John
Pombe Magufuli la kufanya usafi na kutunza mazingira katika siku ya Uhuru, 9
Desemba iliyoadhimishwa jana nchini kote.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla juu na chini mwenye miwani akishiriki kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru, yaliyoadhimishwa jana nchini kote.Kwa kupitia siku hiyo, RC Makalla ameagiza wakazi wake na wananchi kuitumia kila siku ya Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa ajili ya mwendelezo wa kufanya usafi ili kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa safi.
Akizungumza jana
mkoani Kilimanjaro, RC Makalla alisema kwamba wananchi wake walijitokeza kwa
wingi kufanya usafi, huku akiwataka waendeleze kasi yao ya kuhakikisha kwamba
mkoa wao unakuwa safi. Alisema kwa kufanya
hivyo si tu mkoa wao utakuwa safi, ila hata suala la magonjwa ya miripuko
linaweza kuwa hadithi kutokana na kutunza mazingira yao. “Jana nilishirikiana
kwa pamoja na wananchi wangu kufanya usafi, huku nikifanya usafi soko la Memorial,
Hospitali Mawenzi na Soko la Marangu.
“Pamoja na kujitokeza
huko kwa wananchi, naomba suala hili liwe jadi yetu kuanzia ngazi ya kaya,
mtaa, kitongoji na katika maeneo yote,” alisema. RC Makalla aliagiza Halmashauri
zote kuhakikisha masoko yote yanakuwa safi na takataka zinazolewa kwa wakati, bila
kusahau mitaro.
No comments:
Post a Comment