Eneo la ndani la uwanja wa ndege wa KIA.
Aliyekamatwa akiwa na Pembe za Tiwiga ametajwa na idara ya uhamiaji kuwa ni Jasim Mbarakke Alh-kubaisi (43) ambaye anaidaiwa kuwa ni mlinzi wa mfalme wa nchi ya Qatar iliyopo katika falme za kiarabu.
“Ukiangalia haya matukio ndani ya wiki moja ,tumeweza kuokoa kiasicha fedha zisizopungua Bilioni mbili za kitanzania,kama viongozi wengine katika viwanja vingine ,mipakani a taasisi nyingine ila mmoja atashuhudia serikkali yetu inavyoweza kujiondesha kwa kodi za ndani”aliongeza Murusuri.
Alisema katika uwanja huo kumekuwa na matukio mengi ambayo hayakuripotiwa kwenye vyombo vya habari yakiwemo ya kukamatwa kwa watu 11 wakisafirisha dawa za kulevya katika kipndi cha miaka miwli iliyopita.
“Matukio yamekuwa yakitokea mengi ,ndani ya miaka miwili iliyopita katika uwanja huu tumekamata watu wasio pungua 11 wakijaribu kupitisha dawa za kulevya na tayari wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria ikiwemo wengine kufungwa jela.”alisema Mrusuri.
Murusuri alisema kwa sasa katika uwanja huo kumefungwa vifaa vya kisasa ambavyo vinahakikisha kwa hakuna mtu anaye pita uwanjani hapo na vitu ambavyo havijaruhusiwa kisheria ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,John Magufuli.
Mapema wiki iliyopita jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lilitoa taarifa ya kushkiliwa kwa watu wanne wakiwamo raia wanne kutoka mataifa tofauti kwa makosa mbalimbali, akiwemo aliyekutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Fulgence Ngonyani alisema tukio la kwanza lilitokea Dec 15 majira ya saa 10.00 alasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo alikamatwa raia wa Vietnam,Hoang Nghia Trung(49) akitaka kusafirisha nyara hizo.
Alisema mtuhumiwa huyo alihifadhi nyara hizo katika mabegi yake ambapo maofisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa KIA walimtilia shaka na kufanya upekuzi katika mabegi yake ndipo walipokuta nyara hizo zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mabegi hayo.
Hata hivyo thamani halisi ya nyara hizo bado haijajulikana na mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikisha mahakamani mara upeleleziutakapokamilika.
Katika tukio jingine ,Anurag Jain(45) raia wa India alikamatwa uwanja wa ndege wa Kia akiwa na madini ghafi aina ya Tanzanite vipande 264 bila kibali akiwa amehifadhi kwenye mabegi yake akielelekea Hong Kong China.
|
No comments:
Post a Comment