NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
CHAMA cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimeipongeza timu ya Temeke kwa kutwaa Ubingwa wa Taifa Wanawake,baada ya kuifunga Pwani kwa bao 1-0,kwenye mchezo wa fainali uliopigwa jumapili ya Januari 31 kwenye dimba la Azam Complez huko Chamazi.

Katika
fainali hiyo iliyohudhuriwa na waziri mwenye dhamana ya michezo Dk.Fenella
Mukangara,imeshuhudiwa Temeke ikijipatia bao lake mnamo dakika ya 66 kupitia kwa mchezaji wao Neema
Paul.
Temeke walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuwafunga ndugu zao Ilala kwa mabao 4-0,huku pwani wakitinga hatua hiyo kwa kuifunga Kigoma mabao 3-2,katika michezo ya nusu fainali.
Mshindi
amejinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili,
wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja katika michuano hiyo.
Mbali
na Temeke kubeba ubingwa huo,pia imefanikiwa kutoa mlinda mlango bora, Belina
Julius aliyezawadiwa kitita cha shilingi 500,000/-.
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliwakutanisha, Ilala dhidi ya Kigoma ambapo ilala imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kushinda mabao 3-0.
Uongozi
wa DRFA,unatoa shukurani kwa mashabiki wa mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya
jirani,ambao wamejitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo,na kuwaomba
waendelee na mfumo huo ili kuleta hamasa kwa wachezaji.
No comments:
Post a Comment