CHAMA cha kandanda mkoa wa Dar es
salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya
vilabu barani afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza na ushindi katika
mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.
Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa raha
watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini,baada ya kuifunga
mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka Botswana BDF 11,mabao yete hayo
yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe
la shirikisho.
Kwa upande wa Azam FC,wao
waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0
yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika mchezo wa
kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Cpmplex Chamazi.
Mwenyekiti wa DRFA, Almas
Kasongo, amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri
waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea
mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha,ni dhahiri
kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.
Kasongo,pia amesema DRFA imeridhishwa
na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo mengine nje ya jiji kwa
kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na kuwapongeza pia viongozi wa
vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha ya dosari ndogo ndogo
zilizojitokeza.
No comments:
Post a Comment