https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, February 22, 2015

Mchezaji wa zamani wa Simba, Christopher Alex afariki Dunia mjini Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHEZAJI wa zamani wa Simba SC, Christopher Alex, amefariki Dunia mkoani Dodoma, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mchezaji huyo anayekumbukwa kutokana na uwezo wake uwanjani, amefariki ikiwa ni baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

Marehemu Christopher Alex, enzi za uhai wake.
Mapema mwaka huu Alex alisikika katika kituo cha redip cha Uhuru FM, akilalamika jinsi viongozi wa soka wa Simba walivyoweza kumtupa kiasi cha kushindwa hata kumjulia hali, licha ya kuichezea timu hiyo kwa moyo wote.

Katika malalamiko yake hayo, alitumia muda mwingi kumuomba pia nahodha wake wa zamani, Selemani Matola, akiamini kuwa alikuwa na uwezo wa kufuatilia suala hilo kwa viongozi wake hao wa zamani wa klabu ya Simba.

Alex ni moja ya wachezaji mahiri wa klabu ya Simba walioitumikia klabu hiyo kwa moyo na mafanikio makubwa. Akiwa uwanjani mwaka 2002, Alexa na wenzake walaifanikiwa kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwaondosha vigogo wa Afrika, tmu ya Zamalek na kuzua  shangwe Tanzania na kwa nchi zote za Afrika Mashariki na Kati.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...