https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, February 16, 2015

Tanzania yaichapa Kenya 5-3 michuano ya beach soccer

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini Mombasa.

Katika mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne  na Mwalimu Akida bao moja .

Kipindi cha kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya 3 na kipindi cha tatu na cha mwishokwa mchezo kimalizika kwa Tanzania kupata mabao 5 Kenya 3.

Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya, itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.

Mchezo wa kwanza utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.
Timu inarejea leo jijini Dar es salaam majira ya saa 11 jioni ikitokea jijini Mombasa nchini Kenya.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...