Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LIGI Kuu
ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja
utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
wenyeji timu ya Azam FC watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo
msimu huu timu ya Young Africans.
Mechi
hiyo no. 141 itachezeshwa na mwamuzi wa kati Jacob Adongo kutoka Mara,
akisaidiwa na washika vibendera Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma
(Dsm), huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hussein Kalindo (Dsm) na Kamisaa
wa mchezo huo ni Damian Mabena kutoka Tanga.
Katika
mchezo huo timu ya Young Africans itakabidhiwa Kombe lake la Ubingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/2015, na mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr
Fennela Mkangara.
Mchezo
huo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 kamili jioni, kwa saa
za Afrika Mashariki na kati ili kutoa fursa kwa wadau, wapenzi na
mashabiki wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kushudia mchezo huo pamoja
na shamrashamra za kukabidhiwa kikombe.
Young
Africans watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu
na mgeni rasmi, huku wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi
ya Vodacom wakimkabidhi zawadi mchezaji bora wa mwezi Aprili Mrisho
Ngasa na fedha taslimu sh. millioni moja.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika - CAF limewateua waamuzi wa kike kutoka Tanzania kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake U-20 mwaka 2016 kati ya Congo DR dhidi ya Gabon.
Mchezo
huo unatarajiwa kuchezwa jumamosi tarehe 09.05.2015 jijini Kinshasa -
Condo DR, mwamuzi wa kati ni Jonesia Rukya, akisaidiwa na washika
vibendera Dalila Jafari na Sophia Mtongoli huku mwamuzi wa akiba akiwa
ni Hellen Mduma.
Wakati
huo huo Elizabeth Kalinga ameteuliwa kuwa kamisaa wa mchezo kati ya
Kenya dhidi ya Botswana kuwania kufuzu kwa michuani ya Olympiki, mchezo
utakaofanyika Mei 31, 2015 nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment