https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, May 18, 2015

Treni ya Deluxe ya kwenda mkoani Kigoma kuondoka leo saa 2 usiku


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) unasikitika kuwataarifu abiria wa treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma jana Mei 17, 2015 saa 2 usiku kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi leo Jumatatu saa 2 usiku. Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa zinatokana na ajali mbili mfululizo za treni za mizigo.

Ajali ya kwanza ilitokea asubuhi saa 1:30 maeneo ya Stesheni ya Ngeta mkoa wa Pwani na ya pili saa 5 asubuhi maeneo ya Stesheni za Kinguruwila na Morogoro! 

Ajali hizo zimehusisha kuanguka kwa mabehewa manne ( Ngeta ) na kuacha njia behewa moja (Kinguruwila )! Treni zote mbili zilikuwa zikielekea bara! Tayari wahandisi na mafundi wa TRL wako katika maeneo ya tukio kwa ajili ya kazi ya kuyaondosha mabehewa yaliopata ajali na pia kukarabati njia ili ifunguliwe haraka na kurejesha mawasiliano ya njia ya reli katika hali ya kawaida. 


Kutokana na uzito wa kazi hiyo ya ukarabati njia ndio sababu kuu iliyopelekea safari ya Deluxe iahirishwe hadi kesho usiku! Wakati huo huo taarifa imeongeza kusema kuwa ajali hiyo imeathiri urejeshaji wa vichwa viwili vya treni ya Jiji ambavyo havotoweza kufika Dar kwa wakati na hivyo kesho huduma ya treni ya Jiji haitokuwepo. 


Vichwa hivyo vya treni vilikuwa katika ukarabati wa kawaida katika karakana kuu ya TRL Morogoro! Atakayesoma taarifa hii amuarifu nwenzake!
Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza!

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Mei 17, 2015

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...