https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, May 07, 2015

Aliyekuwa Mkurugenzi MUWSA, Cyprian Luhemeja aaga kwa ajili ya kuanza kazi rasmi DAWASC

Aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshu (MUWSA) mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa kauli ya kuwaaga baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Mtendaji mkuu  DAWASCO.
Kauli ya Mhandisi Luhemeja ya kuwaaga wafanyakazi hao ilionekana kama mwiba na kuzua simanzi kuu kwa watumishi hao waliofanya kazi na mkurugenzi huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi 10.
Mhandisi Luhemeja akijaribu kuwapatia wafanyakazi hao Lugha nzuri angalau wasibaki na majonzi.
Meneja Fedha wa MUWSA ,Joyce Msiru akizungumza jambo katika kikao hicho.
Hali ya huzuni ndio ilitawala katika viunga vya ofisi za Mamlaka hiyo.

Na Dixon Busagaga a Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...