https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, May 26, 2015

Bayport: Wa mikoani nao wanaweza kukopa viwanja vya Kibaha


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayaport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo,imesema hata Watanzania wanaoishi mikoani wanaweza kutumia fursa ya kukopeshwa viwanja katika mradi wa Vikuruti, uliopo Kibaha, mkoani Pwani. Unaweza kuptata fomu hapa.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha, Obed Katonge, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliyofanyika mwishoni mwa wiki, katika hoteli ya Serena.

Bonyeza hapa kupata fomu ya mkopo wa viwanja kutoka Bayport Financial Services http://www.kopabayport.co.tz/RESERVATION%20FORM.pdf

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua huduma ya mikopo ya viwanja katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyyo atoke Dar es Salaam au Kibaha.
Kicheko cha furaha. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akifurahia jambo na Meneja Masoko na Mawasiliaano wa Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam.

Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio maana wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali, bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.

“Nafasi ni chache, maana maombi yetu yanafanyika kwa siku (20), kuanzia ile Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services, bila kusahau kupitia bank of Africa (BOA), ambapo malilipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.
“Fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi yetu ya Bayport zilizoenea nchi nzima, huku baada ya Juni 10, mteja akitakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka Bayport, ambapo watumishi wa umma na wa kampuni wanaweza kukopeshwa kiwanja na wakikabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90), baada ya kukamilisha mkopo wake kwa wateja wa fedha taslimu na wengineo wakipewa baada ya kumaliza mkopo wao,” alisema Cheyo.

Kwa mujibu wa Cheyo, huduma ya mikopo ya viwanja ni maalum kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania wote waliokuwa wakitatizwa na suala zima la makazi, hususan kutokana na ugumu wa maisha unaowakumba Watanzania wengi nchini.

Ngula alisema kukaa mikoani si sababu ya  kushindwa kukopa kiwanja kwa sababu wamefungua matawi katika wilaya na mikoa mbalimbali, hivyo ni jukumu la mjasiriamali, mtumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi wanatumia nafasi hiyo kujiendeleza kwa kupata viwanja hivyo.

Naye Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, aliliambia gazeti hili kuwa ukubwa wa viwanja hivyo unaanzia hatua 15 kwa 16, huku thamani yake ikianzia Sh 1,400,000 bila riba (mortgage), ambapo pia fomu zao zimejieleza na kujifafanua vizuri kwa ajili ya kutoa urahisi wa kuwahudumia Watanzania wote.

Mndeme alimaliza kwa kuwataka wateja wao na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuchangamkia viwanja hivyo vinavyokadiliwa kuwa 1878 vilivyokuwa katika eneo zuri, kilomita 50 kutoka Kisutu, jijini Dar es Salaam na kilomita 6.5 kutoka barabara Kuu ya Morogoro.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...