Licha ya mtaa wa Mbweni JKT, jijini Dar es Salaam kujengwa majumba ya kifahari na kupatikana pia nyumba za viongozi mbalimbali wa serikali, miundo mbinu yake, hususan daraja linalojengwa katika eneo hilo ili kuwafanya wananchi wapite kwa urahisi kusua sua. Kwa miaka kadhaa sasa ujenzi wa daraja hilo umesimama.
Pichani ni gari la mwananchi na mkazi wa eneo hilo akipta kwenye maji ambayo mara kadhaa hujikuta wamesimama kwa saa kadhaa, hususan kama eneo hilo litajaa baada ya eneo hilo kujaa maji yanayotoka baharini.
Hali hiyo si tu inakwamisha maendeleo, pia ni hatari kwa usalama wa wananchi kwenye eneo hilo. Wananchi wengi wameonekana kuichoka hali hiyo na kuiomba serikali kulifanyia kazi daraja hilo ili kuwafanya wananchi waingie na kutoka bila usumbufu wowote kama unaotokea wakati huu.
Kambi ya JKT Mbweni ikiwa tulii. Ujenzi wa daraja hilo umekwama. Wananchi hawajui ujenzi huo umekwamia wapi. Baadhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu walimuomba Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda na Mkurugenzi wake kuangalia namna gani mradi huo umesimama kwa miaka mitatu sasa.
No comments:
Post a Comment