Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limesema linatambua uhalali wa uongozi wa sasa wa timu ya Stand United ambapo viongozi wake wamepatikana hivi karibuni baada ya kufanyika kwa uchaguzi ambao awali ulizua utata na kuleta sintofahamu kwa wanachama wake na kufikia hatua ya kusimamishwa kwa chaguzi hizo mbili kati ya Stand United wanaojiita wanachama halali na wa kampuni.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa uhalali wa uongozi huo umekubaliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF iliyokutana Julai 13 kwani kuwa uongozi huo unatambulika kihalali baada ya kujiridhisha na jina la usajili la klabu hiyo iliyosajiliwa kwa jina la Stand United Football Club.
"Uchaguzi uliofanyika ni wa haki na TFF tunatambua uhalali wa uongozi uliopo madarakani kwa sasa", amesema Alfred. Pia uongozi huo wa Stand unatambuliwa mara baada ya kufanya marekebisho ya daftari lake wa wanachama kama walivyoagizwa na TFF.
Amesema kwa wale ambao hawakushiriki uchaguzi huo (Stand kampuni) watabaki kuwa wanachama halali wa klabu hiyo hasa wale ambao walienda upande wa kampuni.
Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya uchaguzi wa TFF walipokutana na kuangalia kanuni na katiba na kufikia muafaka wa kuuhalalaisha uchaguzi huo pamoja na Stand United Fc Wakiwa chini ya Makamu mwenyekiti Domina Madeali
No comments:
Post a Comment