https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, November 13, 2012

Madee akana mpango wa kukimbia Tip Top ‘Connection’



 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Ahmad Ally ‘Madee’, amesema ni ujinga kama ataamua kulikimbia kundi aliloasisi mwenyewe la Tip Top ‘Connection’ la Manzese, jijini Dar es Salaam kama wanavyozusha baadhi ya wadau wa muziki huo nchini.

Habari za Madee kulihama kundi hilo zilienea wiki kadhaa zilizopita na kugusa watu wengi, jambo ambalo hata hivyo limedaiwa kupikwa na watu wasiokuwa na nia njema na kundi hilo linalotesa katika muziki huo nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Madee alisema kwamba kama ataamua kukimbia kundi hilo, ni wazi atakuwa amefanya kitu cha kushangaza,  maana yeye ni miongoni mwa waasisi wake hivyo hawezi kuchukua uamuzi huo.

Alisema kama kutakuwa na tofauti miongoni mwa wasanii, atakachofanya ni kuwekana sawa lakini sio uamuzi wa kuhama na kufanya muziki nje ya kundi hilo kwa madai kuwa haliwezi kumjenga zaidi ya kumbomoa kisanaa.

“Nimekuwa mwasisi wa kundi la Tip Top Connection hivyo kamwe siwezi kuhama kama wanavyosema baadhi ya watu ambao hawaangilii wapi tunapotoka na tunapokwenda katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya.

“Siwezi kuhama Top Top na kama kutakuwa na tofauti nitakuwa mwepesi kukaa na kulizungumzia na sio uamuzi huo ambao daima najua utafanywa kwa ajili ya kuliangamiza kundi hili lenye umri mrefu kwa sasa,” alisema Madee.

Tip Top licha ya kuwa na wasanii mahiri katika kona ya muziki huo nchini, lakini limekuwa likikabiriwa na changamoto za wasanii wake kulihama kwa sababu mbalimbali, yakiwamo maslahi kama yanavyodaiwa na wahanga wenyewe.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...