https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, November 16, 2016

Rais Mstaafu Dr Jakaya Kikwete atunuku digrii ya awali DUCE

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha  Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.

Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190. Picha kwa hisani ya Richard Mwaikenda.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuwatunuku digrii ya awali ya elimu ya jamii  na ualimu  wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo jioni. Jumla ya wanafunzi 864 walitunukiwa digrii hiyo.

 wakivaa kofia zao.
 Wakifurahi kwa kucheza muziki.
 Ni shangwe na vigelegele.
 Mhitimu Bora wa Kike akipatiwa zawadi.
 Warda Jumanne akipatiwa zawadi ya kuwa mmoja wa wanafunzi Bora wa Kike
 Mwanafunzi Bora wa Jumla Haji Mohamed akionesha cheti chake
Makamu Mkuu wa UDSM, akifurahi wakati wimbo wa kabila la wahaya wa Akanana Kaile Kona ukipigwa wakati wa mahafali hayo
 Ni muziki kwa kwenda mbele.



 Eva akipatiwa tuzo ya mwanafunzi bora wa kike.
Mwanafunzi Bora wa Kike Gaudencia Mwita akielekea kutuzwa zawadi maalumu ya Mkuu wa Chuo.
Mwanafunzi Bora wa Jumla wa Duce, Haji Mohamed akitoa hotuba ya shukrani kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu.
 Dk. Kikwete akifurahia jambo na Ngumbullu.
 JK akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo hicho.
Wananchi wakiwa na kamera tayari kuwapiga picha ndugu zao waliohitimu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...