https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, November 02, 2016

Mjengoni band yaanzishwa rasmi jijini Arusha

mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
Wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni  klabu pamoja na mjengoni band wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza)

Habari na picha na Woinde Shizza, Arusha
Bendi mpya  ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni Bandi  imezinduliwa rasmi mkoani Arusha  huku ikiwaaidi mema wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia ndani ya jiji hilo

Akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi rasmi wa bendi hiyo Rais wa bendi  Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa wamejipanga kufanya mkoa wa Arusha kuwa na bendi kubwa inayotoa burudani ya nguvu kama zilivyo bandi zingine za jiji la Dar es salaam akatolea mfano FM Academia na malaika bendi.

Alisema kuwa wakazi wa mikoani wamekuwa wakitegemea bendi kutoka jijini dar lakini kwa sasa  ivi wamesogezewa burudani karibu kabisa na itakuwa kila siku za wekendi
 Bendi mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo
 mashabiki na wapenzi wa  bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii


 Msaniii wa bendi ya Fm Academia Kingombe Blaise na aliuthuria katika uzinduzi huu wa bandi ya mjengoni pamoja na klabu mpya matata ya Mjengoni

 Mmiliki wa blog ya libenee la kaskazini Woinde Shizza  wa kwanza kulia  nyuma yake ni mmiliki  wa blog ya Jamii blog Pamela mollel  ,wakanza kushoto ni dada Fatuma  wa Stax Tv pamoja na Veronica Ignatus  wote tulibahatika kuhuthuria na kushuhudia uzinduzi rasmi wa bendi ya mjengoni  pamoja na klabu ya mjengoni
 Jiji la Arusha kwa nyama ni penyewe na  pia klabu ya mjengoni kwa kuchoma nyama nzuri ndio pamonaongoza wadau wengi walionekana kuvutiwa na  nyama ilikuwa imechoma na wataaalam wa klabu hiyo
Rais wa bendi  Robert Mukongya (Digital) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliouthuria uzinduzi huo
 Burudani ikiendelea  kutoka kwa bendi ya mjengoni








 mmiliki wa jamii blog Pamela mollel akiwa anafafanua jambo kuhusiana na kiota iki kipya kilichozinduliwa rasmi jijini Arusha ambapo alitumia muda huo kuwa sihi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na wale wageni ambao wanauthuria katika  mkoa huu kutoacha kufika mjengoni klabu kwa ajili ya kujipatia nyama choma safi na freshi pamoja na muziki muzuri kutoka katiak bendi ya mjengoni

 Aidha alibaiisha kuwa bendi hiyo anayoisimania inawanamziki wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu  pamoja na uzoefu wakutosha ivyo anaamini wapenzi wa mziki wa dance wataipenda bendi hiyo na kuikubali



Alisema adi sasa bendi na inanyimbo zake na wanajipanga kwa ajili ya kurekodi ili wapenzi ,wadau na wananchi waweze kupata mziki  na kuhusikia katika maredio na hata wanapokuwa majumbani



Alimalizia kwakusema kuwa bendi hiyo ya mjengoni itakuwa inatoa burudani kila wekendi  hivyo wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia wajitokeze kuja kupata burudani ya nguvu inayotoka kwa wanamuziki wa bendi hiyo.



Kwa upande wake wa mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John mdeme  alisema kuwa ameamua kufungua kiota ichikipya ili wakazi wa jiji la arusha wawez e kupata sehemu ya kistaarabu ya kupata chakula ,nyama choma nzuri pamoja na mziki mzuri wa live bandi



Alisema kuwa kimepita kipindi kirefu wakazi wa jiji la Arusha wamekuwa wanakosa sehemu ya kwenda kupata burudani nzuri ya mziki wa bakurutu pamoja na live bendi inayoeleweka tangu hotel ya sabasaba ifungwe ivyo ameamua kuileta burudani hiyo ili wananchi wa Arusha waweze kupata sehemu ya kustarehe



Alimewakaribisha  wageni kutoka mikoani pindi wanapofika jijini Arusha kutoaacha kuja mjengoni kujipatia burudani ya nguvu kutoka katika bendi ya mjengoni pamoja na nyama choma nzuri na freshi inayotengenezwa na wachoma nyama waliobobea katika sekta hiyo.
 watu wakila bata
 huyu ndio mpiga kinanda



Rais wa Bendi ya Mjengoni akiimba kwa hisia




No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...