Na Mwandishi Wetu, Mbeya.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Wilaya ya
Mbeya mjini, kimeingia kwenye mgogoro baina ya viongozi na madiwani.
Mgogoro huo, ambao unatajwa kujikita zaidi kwenye maslahi binafsi ya
watu, huenda ukakiathiri chama hicho kwa kutengeneza mpasuko, kama uongozi wa
juu hautachukua hatua za haraka.
Chanzo cha mgogoro huo,unadaiwa
umetokana na viongozi wa chama hicho kujaribu kutengeneza mazingira ya kuwafuta
uanachama baadhi ya madiwani kutokana na mienendo ya utendaji kazi wao
kutoridhisha.
Inatajwa kuwa chama
hicho, hakikuridhishwa na utendaji kazi wa madiwani hao hivyo kuwaandikia barua
yenye kumbu kumbu namba
CDM/MBY/11/2016/41 iliyosainiwa na Kaimu Katibu Raphael Mwaitege
inayowataka kuhudhuria mkutano mkuu wa
wilaya mbeya mjini.
Pia,Madiwani wote
wametakiwa kutoa maelezo ni kwa nini
hawakuudhulia kikao kilichopita cha tarehe 28/9/2016, kushindwa kushiriki
shughuli za kijamii kama vile misiba, kutaja idadi ya vikao vya baraza
walivyoshiriki pamoja michango ya kifedha waliyokichangia chama.
Mratibu wa Kanda ya
Nyanda za juu Kusini(CHADEMA), Franky Mwaisumbe, amesema ofisi baada ya kupokea
taarifa hiyo iliunda tume ili kufanya uchunguzi wa madai hayo na kwamba imeanza
kufanya kazi November 14, mwaka huu.
Kazi kubwa itakayofanywa
na tume hiyo ni kuwaita na kuwahoji
madiwani wanaotuhumiwa, kuwahoji wananchi juu ya utendaji kazi wa madiwani wao.
Mwenyekiti wa Chadema
Wilaya Obadia Mwaipalu alipohojiwa kuhusu mkanganyiko huo, alikana taarifa za
chadema Wilaya kuwaandikia madiwani hao barua kwa lengo la kutaka kuwahoji na
kwamba hakuna mgogoro ndani ya chama hicho.
Huku hayo yakiendelea
kwa upande wa uongozi, baadhi ya madiwani wameeleza kusikitishwa na hatua
za viongozi wa chama ngazi ya Wilaya kujikita katika kutengeneza migogoro ndani
ya chama badala ya kuwapa woa nafasi ya kuwatumikia wananchi ambao ndio
waliofanikisha kuiweka chadema madarakani na kushika halmashauri.
Wamesema, ni mambo mengi
yamekuwa yakifanywa na uongozi wa juu wa Wilaya ambayo yamekuwa hayana ustawi
mzuri kwa ndani ya chama.
“Kunaviongozi wamefika
mahala, wamekuwa wakidiriki hata kuwatukana kwa kuwarushia matusi ya nguoni
madiwani viti maalum na ukiuliza sababu
huioni, ukiacha hilo viongozi hao wamekuwa wakiwashawishi wenyeviti wa serikali
za mitaa kufanya maandamano wakitaka Meya ajiuzulu kutokana na kushindwa
kushughulikia posho zao,”kilisema chanzo cha habari hii.
Sasa ukiangalia posho za
wenyeviti zinahusisana nini na meya…. kwani licha ya suala lao kushughulikiwa
na mkurugenzi wa halmashauri lakini bado viongozi hao wameendelea kutengeneza
malumbano yasiyokuwa na tija.
Tunafahamu kinachotakiwa
hapa ni nafasi ya Umeya na si kingine
lakini ni vema taratibu zikafuatwa kuliko kutengeneza skendo zisizokuwa
na maslahi kwa chama na kwa wananchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment