Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi pichani, amemuagiza Murugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kumvua madaraka Mratibu wa TASAF wa wilaya hiyo Onesmo Kweyamba kutokana ni kasoro mbalimbali zilizosababishs upotevu wa fedha za serikali kwa kuwapatia kaya ambazo hazikustahili kupewa kupitia mradi wa TASAF.Aidha, wawakilishi 537 wa kaya wamemelipwa kiasi cha Shilingi 266,008,000/= huku wahusika waliokua wakipokea pesa hizo kushindwa kujulikana makazi yao yalipo baada ya uhakiki kufanyika.
Ulipaji wa watu hao umeelezwa kusimamishwa hadi uhakiki mwingine utakapofanyika kwa kushirikisha vyombo vya dola na kubainisha zilipo kaya hizo ili kujua kama zina sifa za kupewa fedha hizo au la. Baadhi ya waliokuwa wakilipwa fedha hizo za kaya masikini ni pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali, sekta binafsi na watu wenye biashara mbalimbali zinazowaingizia kipato kinyume na masharti ya TASAF.
Aidha, wananchi wote wasio na sifa ambao wamekua wakipokea fedha hizi, watawajibika kuzirejesha zote." Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameagiza wananchi wote ambao wana sifa za kupatiwa ruzuku hiyo ya TASAF waingizwe kwenye orodha baada ya wale wasiostahili kuondolewa. Hapi ameagiza hatua nyingine za uchunguzi na nidhamu kwa mujibu wa sheria kuanza mara moja dhidi ya aliyekua mratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi Mh.Hapi amesema fedha taslimu kiasi cha milioni 180,323,000/= zililipwa kwa kaya 515 ambazo hazikua na sifa za kulipwa kulingana na sifa zilizoainishwa huku wananchi wenye sifa wakiachwa.
Hapi amesema, jumla ya kaya 1397 zimebainika kuwa na upungufu wa sifa za kupatiwa fedha hizo za mradi wa TASAF katika wilaya ya Kinondoni na hivyo kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.
Mkuu huyo wa wilaya ameagiza vyombo vya dola wilayani Kinondoni kuanza uchunguzi mara moja dhidi ya wale wote walioshiriki kuhujumu fedha za serikali na kufanya udanganyifu huo kwa awamu saba tofauti za malipo yaliyofanyika tangu July, 2015. "Nimeagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili kubaini udanganyifu wote uliofanyika, na wahusika wote wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment