https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, June 23, 2015

Bayport Financial Services yamfuta machozi Latifa Juma kwa kumpa hundi ya Bima ya Sh Milioni 3

Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto akimkabidhi hundi Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

Na Mwandishi Wwetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, leo jioni imemkabidhi hundi ya Sh Milioni tatu (3,000,000), mjasiriamali Latifa Juma, ikiwa ni sehemu ya mafao yake baada ya mzazi wake Said Juma, kuwa mteja wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao iliyoanzishwa mapema mwaka jana.

Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Bayport Financial Services, Morocco, jijini Dar es Salaam, huku akisindikizwa na mumewe Bakari Msumi. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba marehemu Said Juma alikuwa mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo leo imemnufaisha mtoto wake.

Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto, akiwa kwenye makabidhiano ya hundi Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

Alisema mapema mwaka huu mteja wao alifariki Dunia, hivyo baada ya kupata taarifa hizo tuliamua kufuatilia na kukutana na mtoto wake Ratifa, ambaye hapana shaka fao hili linaweza kumuendeleza zaidi na zaidi. “Bayport Financial Services kama kawaida yetu tumekuwa na lengo la kuwakomboa wateja wetu kwa kuwapatia mikopo mbalimbali kama vile mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa ikiwamo huduma yetu mpya ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, bila kusahau fao la Bima ya Elimu ambalo lina umuhimu mkubwa.

“Naomba Watanzania wote waweke utaratibu wa kujiunga na bima hii ambayo malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000, huku Makato ya bima ya Silver yakiwa ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi,” alisema Ruth.
Naye Ratifa aliwashukuru Bayport kwa huduma zao nzuri, huku akisema mafao ya baba yake yatachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha yake na mama yake, hususan kwa kuendeleza ujenzi wa nyumba yao.
“Ninachotaka kufanya ni kuendeleza ujenzi wa nyumba yetu ili mimi na mama yangu tuishi vizuri, baada ya kufiwa na baba yetu, ambaye leo tumepewa kiasi hicho cha pesa,” alisema.
Naye mume wa Ratifa, Bakari Msumi, alisema hajawahi kuona taasisi yenye huduma nzuri kama Bayport Financial Services, hasa baada ya kuhakikishiwa malipo ya mafao yam zee wao bila usumbufu wowote, jambo ambalo ni nadra kwa taasisi nyingi nchini.

“Awali hatujafahamu kama tunaweza kupata bila usumbufu, ajabu ni kuona sisi tunapigiwa simu hatua kwa hatua, kuelekezwa njia za kupita, hususan baada ya kuitwa katika makabidhiano ya hundi,” alisema Msumi na kuwapongeza Bayport, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia huduma zote zinazotolewa na Bayport. 

Aidha, utaratibu wa malipo ya huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao umepangwa kulipwa kila mwaka, ili kuhakikisha kuwa mafao hayo yananufaisha walengwa, hususan kwa wale wanaoendelea na masomo katika shule na vyuo mbalimbali nchini.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...