https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, February 25, 2016

Benki ya Amana yazindua tawi lake Mbagala

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya Amana, wakati alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi hilo lililofunguliwa leo Feb 25, 2016 Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo, Dkt. Muhsin Salim Masoud (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Al- Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, akisoma hotuba yake ya uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Amana lililofunguliwa Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Kijaji alimwakilisha Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwenye uzinduzi huo.

Monday, February 22, 2016

Bayport yazindua miradi sita ya mikopo ya viwanja, serikali yapongeza

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na taasisi yao katika maeneo sita ambayo ni Kilwa, Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore kutoka kwenye kampuni yao ya BlackWood na Mwanasheria wao Ntiiba Muganga. Picha na Story kwa Hisani ya Bayport Financial Services.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, imezindua miradi sita mipya ya mikopo ya viwanja katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Temeke, Kilwa na Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti kuungwa mkono Watanzania wengi.

Kuzinduliwa kwa huduma hizo mpya za viwanja huku wakiongozwa na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Bertha Minga, kunatanua wigo wa urahisishaji wa maisha ya Watanzania, hususan katika suala la ardhi linalozidi kupanda thamani siku hadi siku, jambo linalohitaji juhudi za taasisi kama Bayport za kuwasaidia wananchi wake kupata maeneo ya makazi kwa utaratibu rahisi na nafuu.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Bertha Minga, aliyesimama akizungumza katika uzinduzi wa hudumaya viwanja inayotolewa na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, leo mchana katika Ukumbi wa Ramada Encore, Posta, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood, Ntiiba Muganga na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood Zahra Moore.

Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo mipya ya viwanja, Mkurugenzi Mkuu Bayport Financial Services, John Mbaha, alisema huduma zao zitakuwa na njia rahisi kwa ajili ya

Saturday, February 20, 2016

Ni hatari, Yanga yaitandika Simba bao 2-0 Uwanja wa Taifa leo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MASHABIKI na wanachama wa klabu ya Simba, leo watalala wakiwa hoi bin taabani baada ya timu yao kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga, mpira uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mechi uwanjani.
Mabao hayo yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili katika mechi hiyo ya kusisimua ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 na Amis Tambwe dakika ya 72 ya mchezo huo.

Hata hivyo Yanga wametumia udhaifu wa hasimu wao kutolewa kwa kadi nyekundu mchezaji wao Abdi Banda na kuifanya timu hiyo ipate unafuu wa kuifunga Simba.

Mpira ulikuwa wa ushindani wa pande zote mbili katika ya kwanza hadi ya 25. Hata hivyo licha ya kufungwa mabao hayo, lakini Simba walitulia zaidi kipindi cha pili, maana wamepata kona 8, huku Yanga wao wakipata kona moja tu na mashuti yaliyolenga goli yaliyopigwa na Yanga yakiwa sita na Simba wao wakipiga mashuti matano.


Hadi mpira unamalizika, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya mtani wao wa jadi Simba.

Monday, February 15, 2016

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mabalozi wapya watatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau. Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Hashim Lundenga ambeba mgongoni Hoyce Temu

Hashim Lundenga
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (pichani) amezungumza na mtandao huu kuhusu habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kumhusu Miss Tanzania 1999, Hoyce Tamu. Lundenga amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania na Mtanzania wa kawaida amesikitishwa na maneno hayo na kuwa hayapendezi kusemwa kwa mtu kama Hoyce ambaye amejitoa kusaidia jamii.

Alisema kuwa anashangazwa na mtu ambaye amekuwa akiandika maneno hayo mtandaoni kwani hawakuwa na utofauti wowote na kilichokifanya ni kumuandika Hoyce ambaye hakuhusika katika ugomvi uliokuwepo baina ya mtu huyo na mdogo wake Hoyce, Rachel.
“Nimesikia habari hizo kumhusu Hoyce kwa kweli nimesikitishwa sana, sio jambo zuri ambalo amelifanya huyo aliyemuandika,” alisema Lundenga.

Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka watumiaji wa mtandao kuwa na matumizi mazuri ya mtandao ili kuzidi kuifanya mitandao ya kijamii kuwa sehemu salama kwa ndugu na marafiki kuwasiliana.

Bondia Said Mbelwa kuvaana na Ibrahim Tamba, Machi 26 Dar es Salaam

Promota Jaffari Kitemo 'katikati' akiwainua mikono juu mabondia Ibrahimu Tamba kushoto na Said Mbelwa wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana utakaofanyika march 26 katika ukumbi wa frends corner Manzese, Dar es Salaam. 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABONDIA Ibrahimu Tamba na Said Mbelwa jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 26 katika ukumbi wa Frends corner manzese Dar es salaam, mpambano uho wa raund nane kg 76 umeratibiwa na  Jaffari Kitemo.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mikataba ya kuzipiga Kitemo alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ukiondoa pambano hili na tumeandaa mpambano uhu kwa ajili ya kuondoa ubishi wa nani zaidi mana kila mmoja anatamba mtaani kuwa yeye ni zaidi ya mwenzie sasa jibu tutalipata Machi 26 pale Manzese

Naye bondia Mbelwa amesema kuwa kawaida yake ni kugawa dozi kwa kumpatia kipigo kitakatifu Tamba akijibu majigambo hayo Tamba amesema mkuwa yeye ana makuu huvyo atakikisha anafanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kumpiga Mbelwa kwani ngumi ni ngumi tu.

Mwanachama wa Coastal Union Hafidh Kido asema mwenyekiti wao ni jipu

Niliamua kukaa kimya kuhusu kinachoendelea katika Klabu ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ hasa katika kipindi hiki tunachopambana tusishuke daraja. Uzalendo umenishinda.
Niliwahi kuwa msemaji wa timu, lakini mbali ya utumishi huo ndani ya nafsi yangu ninaipenda Coastal Union. Natamani siku zote iwe inanipa raha hata nikikaa na wenzangu nijisifie kuzaliwa Tanga.

Mdau wa soka na mwanachama wa klabu ya Coastal Union, Hafidh Kido, pichani.
Kuna kitu wengi hawakijui, Coastal Union iliyoanzishwa mwaka (1948) ni miongoni mwa timu zilizofanya vizuri katika miaka ya mwanzo ya kuanzishwa ligi kuu wakati huo ikiitwa ligi daraja la kwanza.  Hata Simba na Yanga hazikufua dafu, katika miaka ya mwanzoni baada ya uhuru timu zilizokuwa zikishika nafasi za juu katika msimamo wa ligi ni Simba, Yanga, African Sports na Coastal Union. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, timu za Tanga zinaonekana kituko.

Tulishawahi kukaa chini tukajadiliana tatizo ni nini, majibu tuliyopata ni uongozi; hiyo ni baada ya kupima vitu vinne, Kocha, Mashabiki, Wachezaji na Uongozi. Tulipoangalia morali ya mashabiki tukabaini ipo juu, maana yake kila mechi hamasa inatolewa. Tukaangalia nafasi ya wachezaji labda hawana uwezo, tukabaini wachezaji kuna baadhi ya mechi wakiamua kukaza wanapata ushindi, maana yake uwezo wanao.


Tukaangalia upande wa makocha, wengi baada ya kutimuliwa walifanya vizuri katika timu walizokwenda, tukianzia na Yusuf Chippo, Juma Mgunda, Hemed Morocco, Ally Jangalu, Mayanja na wengine wengi ambao walipita Tanga wakaonekana wabovu lakini baadaye walifanya vizuri kwengine.

Friday, February 12, 2016

Milioni 20 zazua balaa msikitini

Waumini wa dini ya Kiislam wakizozana nje ya Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam katika swala ya Ijumaa leo mchana, baada ya kutokea tafrani ya waumini hao dhidi ya viongozi wao ambao wanatuhumiwa kutafuna fedha zaidi ya sh.milioni 20 walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
Muumini wa Msikiti huo, Mbarouk Mohamed Makame (kushoto), akizungumza kuhusu fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao. Kulia ni mmoja wa wazee wa msikiti huo, Mzee Selasela.

Waziri Jenister mhagama afunga mkutano wa 25 wa PPF




Waziri wa Sera, Bunge, Vijana Ajira na Walemavu Jenista Mhagama, akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni PPF, uliomalizika leo Feb 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani/MafotoMedia. 
Wadau wa Mfuko huo wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri Jenista Mhagama.

Thursday, February 04, 2016

Bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi kuparuana Sikukuu ya Pasaka

Mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es salaam. Mratibu wa mpambano huo ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'.
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya Sikukuu ya Pasaka katika Uwanja wa Ndani wa  Taifa, ukiwa ni mpambano wa raundi nane KG 76.
Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo, kocha wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano huo amesema kuwa amewasainisha mabondia hao wanaotamba katika mchezo wa masumbwi nchini.
Mratibu wa mpambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka utakaofanyika  uwanja wa ndani wa Taifa.

FOS yatoa ripoti ya ushirikishwami wa wanawake kwenye Uchaguzi Mkuu

Meneja wa Mradi wa kitengo cha haki Jinsia kutoka Oxfam Bi. Rishida shariff akielezea kwa kina namna walivyofanya mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa
 Mtafiti mkuu wa kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Profesa Ruth Meena akifafanua kwa kina namna ya utafiti ulivyofanyika.

Wednesday, February 03, 2016

Mchaka mchaka wa kuondosha simu feki Tanzania wazidi kupamba moto

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.

Barabara mbovu yawatoa chozi wananchi wa Mnyonzole/Kibesa

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
WAKAZI na wananchi wa vijiji vinavyounda Kata ya Panzuo,  wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, wameendelea kuililia barabara mbovu inayoanzia Kijiji cha Kimanzichana, hali inayowalazimu akina mama kujifungulia njiani na kuuweka uhai wao rehani.
Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana, kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa,wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, nauli kwa safari moja wakitoza Sh 20,000 hadi 30,000 kwa safari moja. Nyakati za mvua barabara hiyo haipitiki hali inayozidisha ugumu wa maisha kwa wananchi hao.

Vijiji hivyo ni Marui, Kisegese, Mbezi Muungwana, Msanga Visiga, Kibayani na vinginevyo vinavyoitumia barabara hiyo inayopitika wakati wa jua kali na zinapoanza mvua mawawasiliano yao kutoka katika maeneo yao hadi kwenye barabara Kuu ya Lindi Dar es Salaam kukosekana.
Mkazi wa kijiji cha Mnyonzole Kibesa, Cosmas Kisabo, akizungumza jambo kuhusiana na kero kubwa ya barabara wanayokutana nayo wananchi hao, inayaopelekea akina mama wengi kujifungulia njiani, mvua kubwa zinapoanza kunyesha.

Mwandishi wa mtandao huu ametembelea katika maeneo hayo na kujionea hali mbaya ya barabara hiyo ambayo inaweza kuwa chanzo cha kuinua uchumi wa wananchi hao endapo itakarabatiwa japo kwa kiwango cha changarawe ngumu.

Akizungumza jana wilayani hapa, dereva wa bodaboda anayejulikana kama Ramadhan Rajab, alisema kwamba mvua kubwa inaponyesha huwezi kutoka ulipokuwa kwenda sehemu yoyote, kwa sababu barabara inakuwa mbovu.
Mkazi wa kijiji cha Kibesa, Bi Sofia Michael anayejishughulisha na kilimo na biashara ndogo ndogo, akiwa nje ya kibanda chake akizungumza na mtandao huu. Bi Sofia anasema maisha yamekuwa magumu zaidi kutokana na kukosa barabara.

“Watu wa huku tunaishi magumu mno, maana hata sisi wa bodaboda hatuwezi kufanya kazi zetu vizuri ukizingatia kuwa watu wengi wanaoishi mjini wakija kwetu tunawasafirisha katika

Tuesday, February 02, 2016

Unilever yaendelea kuwazawadia wanafunzi shule mbambali Dar

Mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Maarifa, Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam  Ester Lawrence akipokea fulana kutoka kwa Balozi wa Blue Band Neema Upendo shuleni hapo jana akiwa ni mmoja wa washindi wa shindano la Blue Band ‘Kula Tano’ linalowamasisha wanafunzi kutambua umuhimu wa kula vyakula vyenye virutubisho. Kushoto ni mwalimu wa michezo Edith Katundu.

Mkuu wa wilaya Kinondoni aendelea kupokea mifuko ya cement ya msaada kujengea shule

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500. 
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.

Monday, February 01, 2016

Mahakimu 508 wawekwa kikaangoni nchini Tanzania

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.

Na Dotto Mwaibale
JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508  watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango. Jaji Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.

Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana. Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu  wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.

Thursday, January 28, 2016

Picha mbalimbali zinazoonyesha athari ya mvua jijini Dar es Salaam

 Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.
 Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo  kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.

Pitia tamko lote la Chama cha CUF kususia Uchaguzi wa marudiano visiwani Zanzibar

IMG-20160128-WA0019
AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.
Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

Wakabidhiwa jengo la mafunzo na madawati Kilombero

 Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi  jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa  5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
 Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero

Mtandao wa Kenya umetoa uongo wa Rais Magufuli kutembelea Kenya

Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii. 
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanhabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe. 
Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo! 
Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

Sunday, January 24, 2016

Rais John Pombe Magufuli atunuku Kamisheni Maafisa wapya Monduli

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.

Friday, January 22, 2016

Waziri Ummy Mwalimu azindua duka la dawa la MSD jiji Mwanza

 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.

Nyota wa kikapu wa Malawi kuzikabili timu za Da

 Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
 Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
*************************
Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.

Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.

Friday, January 15, 2016

Esther Bulaya na Steven Wasira wapepetana Bunda

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu. 

Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.

Wednesday, January 13, 2016

Mbunge wa jimbo la Arumeru ajichimbia China kusaka

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa katika moja ya karakana ya kutengeneza vifaa tiba katika mji wa Guangzhou nchini China.

Wateja wa Tigo Pesa kuvuna 4.4bn/- gawio la robo mwaka

Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo, Obedi Laiser akielezea kuhusu gawio la mwaka huu  kwa watumiaji wa Tigo Pesa, kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni inayongoza katika kuleta maisha ya kidijitali kwa jamii, Tigo, imetangaza tena malipo ya robo mwaka ya shilingi bilioni 4.4 (dola milioni 2.1) kwa watumiaji wake wa huduma ya Tigo Pesa wapatao milioni 4.6. 

“Gawio hili la faida linalipwa kwa watumiaji wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wetu wa kibiashara, kila mmoja kutokana na thamani  ya fedha aliyojiwekea katika akaunti yake ya Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao, Obedi Laiser.

 Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Laiser amesema  kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza Tigo kuwalipa gawio la faida watumiaji wa Tigo Pesa kwa mwaka wa 2016  akibainisha kuwa malipo hayo ni faida inayopatikana kutokana na amana ya mfuko wa Tigo Pesa uliyowekezwa katika benki za kibiashara hapa nchini. 

Akamatwa na meno ya tembo kilo 50 mkoani Katavi

Meno ya Tembo vipande 8 vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani  ya milioni  120  ambayo ni sawa na Tembo hai wane aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa  Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. 

Picha  na  Walter Mguluchuma, Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika  kwa jina la  Nzuri  Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede  Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi  amekamatwa akiwa  na meno  ya Tembo  nane  yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari   kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa   mida ya saa tatu  na nusu .
Kidavashari alisema mtuhumiwa  Ndizu  alikamatwa  kufuatia   misako  na  uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa  na Jeshi la Polisi  ikiwa ni kuhakikisha  wahalifu  wa makosa mbalimbali wakimemo  wawindaji  haramu  wa wanyama pori  wanakamatwa.
Mtuhumiwa  Nzuri  Ndizu,  Mkazi wa Kijiji  cha Mbende Wilaya ya Mlele, akiwa katika  ofisi ya Kamanda  wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  baada ya kukamatwa na meno ya Tembo  vipande  nane   yenye thamani ya shilingi  milioni  120  hapo juzi.

Umoja wa Makanisa wafanya maombi mazito Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza

Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema.

Pia maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo.

Tuesday, January 12, 2016

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto akagua jengo la Zahanati kijijini Mpingi


Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi.
Na Mwandishi Wetu, Songea
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la Zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. 

Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa  Bima ya Afya.

Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.

Kamati ya Uendeshaji wa ligi waipa kicheko Polisi Dodoma Ligi Daraja la kwanza

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi umeipa Polisi Dodoma ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mji Mkuu FC kumchezesha mchezaji Peter Ngowi aliyekuwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Desemba 26, 2015 mjini Dodoma.
Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(4) na 14(37) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mji Mkuu FC ilikuwa imeshinda mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa.
Kamishna wa mechi ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Polisi Tabora na Panone FC ya Moshi, Shabani Funyenge amesimamishwa kutokana na ripoti yake ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kuwa na upungufu.
Klabu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu yake kutoa kashfa na lugha za matusi wakati wa mechi ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Kiluvya United iliyofanyika Novemba 8, 2015 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Kaume jijini Dar es Salaam.
Pia imetakiwa kulipa kibendera cha kona (corner flag) pamoja ubao wa matangazo wa geti la kuingilia ndani kwenye Uwanja wa Karume ambavyo vilivunjwa na washabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi hiyo.
Mtunza vifaa wa timu ya Kimondo, Emily Nehemia, Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Idd Kibwana, Kiongozi wa Panone FC, Said watafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.

Serikali yatoa taarifa kwa umma juu ya mwelekeo wa ugonjwa Kipindupindu

DSC_0063
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dkt. Rufaro Chatora

Taarifa kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini ni kama ifuatavyo; Tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua Kipindupindu, na kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huu. Katika kipindi cha wiki iliyoanza tarehe 04 hadi 10 Januari 2016, kumekuwa na jumla ya wagonjwa 615 walioripotiwa nchini kote na vifo vitatu (3). Mikoa ambayo bado imeripoti kuwa na ugonjwa huu ndani ya wiki moja iliyopita ni 11 kati ya 21 iliyokuwa imeripoti ugonjwa hapa nchini. Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma, Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu. Kati ya hiyo, mikoa inayoongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa wapya ndani ya wiki moja iliyopita ni pamoja na Morogoro (Manispaa ya Morogoro 87, Halmashauri ya Morogoro 66), ukifuatiwa na Arusha (Arusha Manispaa 50), Singida (Iramba 40) na Manispaa ya Dodoma ( 33).

Aidha, mikoa iliyokuwa na maambukizi lakini kwa muda wa wiki moja iliyopita hakukuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu ni pamoja na Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Lindi. Vile vile mkoa wa Dar es Salaam ambako ndiko ugonjwa ulianzia na kudumu kwa muda wa miezi minne (4) haujaripoti mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015. Mikoa ambayo ilikwisha kuwa na ugonjwa huo lakini hapajakuwepo na wagonjwa wowote kwa muda wa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa. Pia mikoa ambayo haijawahi kutoa taarifa ya ugonjwa wa kindupindu tangu mlipuko huu uanze hapa nchini ni Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Monday, January 11, 2016

Rais Magufuli amtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Muhimbili kumjulia hali


 
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS



 Na Mwandishi Wetu

BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebela, January 30 katika Ukumbi wa Sativa uliopo Kyela, mkoani Mbeya, mpambano huo wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa huo

Akisaini mkataba huo mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa, amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito huo

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...