https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, February 03, 2016

Mchaka mchaka wa kuondosha simu feki Tanzania wazidi kupamba moto

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji Huduma za Maweasiliano Thadayo Ringo akimsomea ujumbe mmoja wa waandishi wa habari aliyehudhuria mkutano huo baada ya kuweka namba hizo na kuja ujumbe wa simu siyo feki.
Mdau wa habari Farouk Karim akiuliza swali wakati wa mkutano huo kuhusiana na uingiaji wa simu kutoka Ulaya nyingi huwa na lock wakati wa mkutano huo.
Mwandishi Amour Mussa akiuliza kuhusu TCRA inachukua hatua gani endapo simu ikiibiwa.
Ndugu Issa Yussuf akuliza jinsi ya utaratibu wa kuwafikia wananchi wa vijijini na zoezi hilo la ugunduzi wa simu feki ili kuweza kuepuka na hasara utakapofika mwisho wa matumizi ya simu hizo feki. 
Naibu Mkurugenzi Thadayo Ringo akifafanua na kujibu maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na matumizi ya simu feki kufikia mwisho wake wa matumizi Tanzania.
Meneja Mawasiliano TCRA  Innocent Mungy  akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kusitishwa kwa matumizi ya simu feki ifikapo mwezi juni 2016. 
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Zanzibar TCRA Ndg Seif  S Waziri akizungumza wakati wa mkutano huo na kutoa neno la shukrani kwa waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo wa kutoa elimu ya simu feki kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar   
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa mafunzo ya kutambua simu feki na Orijino uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspot.
Zanzinews.com. 

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...