https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 12, 2016

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto akagua jengo la Zahanati kijijini Mpingi


Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi.
Na Mwandishi Wetu, Songea
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la Zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. 

Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa  Bima ya Afya.

Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao.

Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya,  kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi



Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...