https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, July 05, 2017

Phillip Luberege wa Dar es Salaam azoa Sh Milioni 20 za Biko

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FUNDI ujenzi Phillip Luberege mwenye maskani yake Gongolamboto jijini Dar es Salaam, ametangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, akipatikana katika droo ya 20 ya kuwania Sh Milioni 20.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Gongolamboto, Phillip Luberege. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Kajala Masanja kulia akiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Luberege ametangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam katika droo ya 20 iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, akishirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kupatikana kwa washindi wa mikoani kiasi cha kuashiria kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kutoka kona zote za Tanzania kuchangamkia mchezo wao kwa watu kuchangamkia fursa ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.
Alisema kwamba mchezo wao wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, kwa sababu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni yao ni 505050 na kumbukumbu yao ni 2456, huku kiasi cha kuanzia kucheza kikiwa ni Sh 1000 na kuendelea.

“Sh 1000 ya kucheza Biko inampa mshiriki wetu nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo hufanyika Jumatano na Jumapili, huku mpaka sasa Biko ikitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na Juni pekee,” Alisema.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe alisema kwamba maofisa wa Bodi yao wamekuwa wakihudhuria droo zote za Biko, huku wakisema kuwa mchezo huo umekuwa ukichezeshwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote.

“Biko ni mchezo unaofuata sheria zote, hivyo ni salama ambapo kwa wiki hii amepatikana mshindi wa Gongolamboto, baada ya kuchezeshwa droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 ya Jumatano,” Alisema.

Kwa Mwezi Mei na Juni pekee, waendeshaji hao wa mchezo wa kubahaisha wa Biko wametoa zaidi ya Sh Milioni Bilioni moja tangu kuanzishwa kwa mchezo huo unaotikisa katika viunga mbalimbali vya Tanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...