https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, July 23, 2017

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara aibuka na Sh Milioni 20 za Biko


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko katika droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.


Lukinga fundi wa Tanesco alitangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed kushoto akiandika maelezo ya mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 alilopata mfanyakazi wa TANESCO Mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga mara baada ya kupatikana kwenye droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja. Picha na Mpigapicha Wetu.
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha pozi nzito baada ya kupatikana mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyetengazwa katika droo ya 25 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema ni mara ya kwanza kumpata mshindi wa droo kubwa ya Sh Milioni kutoka Mkoa wa Mtwara.


Alisema kupatikana kwa mshindi huyo kunaongeza wigo wa washindi wa Biko kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wanaoshinda droo kubwa pamoja na wanaoibuka na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.


“Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mchezo wetu wa kubahatisha tumempata mshindi kutoka Mtwara, ambaye ni fundi wa Tanesco, huku tukiamini kuwa kila mtu anaweza kuibuka na ushindi kutoka Biko endapo atacheza mara nyingi zaidi kwa kupitia mitandao ya simu.


“Biko inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama za uchezaji zikianzia Sh 1,000 na kuendelea, ambapo shilingi 1000 inatoa nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotolewa kila Jumatano na Jumapili,” Alisema Melles.


Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, alimpongeza Lukinga kwa kuibuka na ushindi huo mnono, huku akisema Biko ni mchezo unaochezwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa katika tasnia ya michezo ya kubahatisha.


“Bodi yetu inakuwa karibu kuhakikisha kwamba washindi wetu wanapatikana kihalali, ambapo safari hii mkazi wa Mtwara, Lukinga ameibuka kidedea kwa kupata donge nono la Biko la Sh Milioni 20,” Alisema.


Naye Lukinga akizungumza kwa simu wakati anahojiana na Kajala, Balozi wa Biko, alisema haamini kabisa kama ameshinda zawadi nono ya Biko, akipigiwa simu kuambiwa hilo dakika chache baada ya namba yake kushinda.


“Nashukuru sana kwa kushinda zawadi hiyo nono kutoka Biko, maana siku ushindi huo umeniaminisha kuwa watu wanashinda kihalali, hivyo huu ni wakati wangu kufurahia maana hata jana nilicheza Biko,” Alisema.


Kwa kushinda donge nono la Biko, Lukinga anatarajia kupokea fedha zake haraka wiki hii, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kutoa zawadi za fedha za papo kwa hapo pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 zinazotolewa Jumatano na Jumapili, huku mwezi Mei na Juni pekee Biko wakitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wao.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...