https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, July 02, 2017

Mjasiriamali Mlandizi mkoani Pwani azoa Milioni 20 za Biko

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, kushoto akizungumza jambo na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja katika kuchezesha droo ya 19 ya Biko ambapo mjasiriamali Elisiana Laizer kutoka Mlandizi, mkoani Pwani alifanikiwa kuwa mshindi wa Sh Milioni 20.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI mdogo wa Mlandizi, mkoani Pwani, Elisiana Laizer, leo  ametangazwa kuwa mshindi wa droo ya 19 ya kuwania Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutikisa hapa nchini.

Droo ya kumpata mwanadada huyo ilichezeshwa jana jijini Dar es Salaam na balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehus Ngolo.

Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba ni furaha yake kuona droo tatu kati ya 19 zilizoendeshwa na Biko zimewapata wanawake watatu, jambo linaloonyesha kwamba mchezo wao umekuwa wa Watanzania wote.

“Ni jambo la kutia moyo kuona droo ya 19 imempata dada wa Mlandizi, Elisiana ambaye anajishughulisha na biashara ndogo ndogo maeneo ya Mlandizi, mkoani Pwani, nikiamini kuwa ni hatua nzuri kwake na Kwa Watanzania wote wanaocheza Biko,” Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Biko imezidi kukolea baada ya kutoka Dodoma, ikaenda Mbeya sasa imetua mkoani Pwani kwa mshindi wao Elisiana ambaye ameibuka kidedea kwa Sh Milioni 20, huku zawadi mbalimbali za Biko za hapo kwa hapo zikianzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Tumetoka Mbeya juzi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wetu Linda Mhewa Sh Milioni 20 zake, huku leo tukimpata msichana mwingine anayeishi Mlandizi, mkoani Pwani aliyecheza Biko mchezo rahisi unaochezwa kwa ujumbe wa simu za mikononi wa Tigo Pesa, M-pesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, alisema Biko ni mchezo rahisi wa ujumbe mfupi wa maandishi unaotoa ushindi kwa Watanzania wote, hivyo Watanzania wachangamkie fursa.

“Biko ni mchezo unaofuata sheria, kanuni na taratibu zote, hivyo tunaomba Watanzania wacheze kwa wingi ili wavune mamilioni ya zawadi kutoka kwenye mchez huu,” Alisema.
Hadi sasa tayari zimeshafanyika droo 19 za kutoa ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20, huku Biko wakitoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa Mwezi Mei pekee tangu mchezo huo wa kubahatisha ulipoasisiwa nchini Tanzania na kutoa fursa ya utajiri kwa Watanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...