https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, July 12, 2017

Milioni 20 za Biko zaenda Morogoro, Lohai naye avuta mkwanja wakeNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DROO ya 22 ya waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku, imefanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Morogoro, Elizabeth Damian akifanikiwa kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 zinazotolewa na bahati nasibu hiyo.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yassin Lohai akipiga picha ya shangwe baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la Madaraka la NMB jijini Tanga leo mchana. Lohai alikabidhiwa na Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven hayupo pichani.

Mwanadada huyo kutoka mkoani Morogoro, alitangazwa mshindi katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.


Akizungumza katika droo hiyo, Kajala aliwataka Watanzania kuendelea kucheza Biko ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuvuna mamilioni yanayotolewa na Biko tangu kuanzishwa kwake, huku hadi sasa kwa miezi miwili ya Mei na Juni, zaidi ya Sh Bilioni moja zikienda kwa washindi.


Alisema fursa inayotolewa na Biko ni nzuri kwa uchumi wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba wanacheza Biko mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, sambamba dau nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili, kianzio cha kucheza kikiwa Sh 1000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ya Biko ikiwa ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa Tanga, Yassin Lohai baada ya kushinda donge nono la Biko Jumapili iliyopita. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Madaraka, jijini Tanga, akishuhudia makabidhiano hayo kwa mshindi wa Biko mkoani Tanga.
Balozi wa Biko Kajala Masanja, kulia akisalimiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, katika droo ya kumtafuta mshindi wa Milioni 20 wa droo ya 22, ambapo Elizabeth Damian alitangazwa mshindi leo asubuhi.


“Tangu Biko ianze kuchezeshwa Tanzania imekuwa ikitoa nafasi kubwa ya Watanzania kuvuna mamilioni, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi kucheza Biko ili nao waweze kuvuna fedha zinazotolewa Biko kwa zawadi za papo kwa hapo pamoja na zile wiki ambazo ndio kubwa zaidi, nikiamini kuwa endapo mtu anafanikiwa kuzipata, naamini atapiga hatua kubwa kiuchumi,” Alisema Kajala.


Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, alisema Biko ni mchezo rahisi na halali unaofuata sheria zote, hivyo wanaamini Watanzania wataendelea kutumia fursa za kucheza mchezo huo wa kubahatisha wa Biko.


“Bodi yetu imekuwa ikihudhuria droo zote za Biko na leo amepatikana mkazi wa Morogoro anayejulikana kwa jina la Elizabeth Damian, hivyo tunampongeza kwa ushindi wake pamoja na kuwahakikishia usalama mkubwa juu ya mchezo huu,” Alisema.


Katika hatua nyingine, mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 21 kutoka mkoani Tanga, Yassin Lohai, leo amekabidhiwa fedha zake, huku akiwashukuru Biko na kuahidi kuwa atazitumia vizuri fedha zake katika hali ya kuziingiza katika harakati za kumletea maendeleo makubwa.


“Nashukuru Mungu kwa kukabidhiwa fedha zangu Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wenzangu kuwa mchezo huu ni kweli washindi wanapewa zawadi zao haraka, jambo linaloweza kutusaidia kutukwamua kiuchumi,” Alisema Lohai na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.


Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alisema kuwa Biko unazidi kuchanja mbuga kwasababu washindi wengi wa papo kwa hapo wamekuwa wakipatikana sambamba na wale wanaoibuka na mamilioni 20 wanaoshinda na kukabidhiwa fedha zao haraka kwa ajili ya kuwapatia mwangaza wa kiuchumi.


Kwa miezi miwili ya Mei na Juni, washindi wa Biko wameshinda na kukabidhiwa fedha zao zaidi ya Sh Bilioni moja, jambo linalotafsiriwa kuwa ni sehemu ya kuwakwamua Watanzania wanaoitumia fursa ya uwapo wa mchezo wa kubahatisha wa Biko unaochezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanyaa miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...