https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, July 25, 2017

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven mwenye fulana ya Biko kushoto akiwa ameshika hundi saa chache kabla ya kumkabidhi kiasi cha fedha cha Sh Milioni 20 mshindi wa Mtwara, Ally Hassan Lukinga katikati. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, jana amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko, jumla ya Sh Milioni 20.


Makabidhiano hayo yamefanyika jana mkoani Mtwara katika benki ya NMB, ambapo Lukinga aliishukuru Biko na kusema kuwa fedha hizo atazitumia vizuri kuhakikisha zinakuza uchumi wake.


“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha hizi ambazo kwa hakika nitazitumia vizuri kama sehemu ya kupiga hatua kiuchumi kama dhamira ya Biko kuanzisha bahati nasibu yao.

Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko Tanzania, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia, akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa mjini Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyeshinda katika droo ya 24 Jumapili. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.

“Awali sikuamini kama naweza kushinda donge nono la Sh Milioni 20, hivyo ni wakati huu Watanzania wote kuamini kwamba Biko ni mchezo wa kubahatisha wa watu wote, maana kama hata mimi wa Mtwara nashinda, ndio kusema yoyote anaweza kushinda,” Alisema.

Ally Hassan Lukinga kulia akifurahia fedha zake alizokabidhiwa na Biko mkoani Mtwara.


Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles, alimpongeza Lukinga kwa kukabidhiwa fedha zake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya Biko ili washinde zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, sambamba na droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka Jumatano na Jumapili.


“Jumapili hii amepata Lukinga ambapo leo tumemkabidhi fedha zake, hivyo wote mnaweza kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ya kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea kikiwa Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema.


Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Biko inaendelea kutoa zawadi mbalimbali zikiwapo za papo kwa hapo na zile za Milioni 20, hivyo yoyote atakayeshinda katika Mkoa wa Tanzania atafikishiwa fedha zake haraka iwezekanavyo ili azitumie kwa ajili ya maendeleo yake.


“Kumpatia fedha zake Lukinga wa mjini Mtwara ni nafasi ya kumsubiri mwingine aibuke na mamilioni ya Biko ili naye apate chake, maana Biko ipo kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo dawa ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi wakati wowote na mahala popote kwenye mikoa yote ya Tanzania,” Alisema.


Baada ya kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Mtwara, mshindi mwingine wa Sh Milioni 20 anatarajiwa kupatikana Jumatano ama (Jumatamu) kama wanavyoita, ikiwa tayari Biko wameshakabidhi zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi ya Mei na Juni pekee.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...