https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, June 28, 2017

Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao


Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde, kulia akiwa na mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mjini Dodoma. Waziri Mavunde amepongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu ili afanikiwe kiuchumi.Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mheshimiwa Anthony Mavunde, amewataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa Dodoma kunufaika kiuchumi kwa kuutumia vyema uwapo wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’.


Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa makabidhiano ya Sh Milioni 20 kutoka kwa mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, ambaye ni fundi cherehani mwenye maskani yake mjini Dodoma, akitangazwa mshindi katika droo ya 17.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde kulia akiwa na wananchi wake wa Dodoma Mjini walioshinda Sh Milioni 20 za Biko kila mmoja. Evodi Mlingi katikati amekabidhiwa fedha zake jana wakati kushoto ni Ramadhan Juma Hussein aliyeshinda Milioni 20 hivi karibuni ambapo tayari ameshapokea fedha zake kutoka Biko.

Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa kwenye tukio la kumkabidhi fedha zake mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, kushoto, mjini Dodoma jana.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Mavunde alisema kwamba serikali ya awamu ya Tano ni ya viwanda, hivyo ni jukumu la washindi hao kuhakikisha kwamba wanaanzisha na kusimamia biashara kubwa kwa kutumia mamilioni ya Biko.


Alisema fedha za Biko zinaweza kutumiwa vizuri na washindi wao, huku katika jimbo lake, mbali na watu kuibuka na ushindi wa papo kwa hapo unaonzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa kwa kupitia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ya Biko 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.


“Nawataka kila mtu ahakikishe kwamba akipata fedha hizi anazitumia vizuri na mimi kama mbunge wao wa Dodoma nitasimamia katika kuwapatia mwangaza mzuri wakati wowote wakihitaji, maana lengo la serikali ni kupiga hatua kiuchumi,” Alisema.


Naye Evodi Mlingi aliwapongeza Biko kwa kuhakikisha kwamba wamemfikishia fedha zake haraka tofauti na matarajio yake, licha ya kuwa na imani kubwa na waendeshaji wa mchezo wa Biko ambao umekuwa ukitoa fedha nyingi kwa washindi wao.


“Nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko kila siku na kila saa ambapo ninapopokea fedha ya ushindi wa papo kwa hapo naipeleka tena Biko jambo ambalo nimepata ushindi mnono kwa kuchanganya na maombi yangu kwa Mungu, maana nina uhitaji mkubwa wa fedha na hizi nilizopata naahidi kuzipeleka kwenye fungu la kumi kama nilivyotaka tangu mwanzo,” Alisema Mlingi huku akiwashauri Watanzania kucheza kwa wingi ili wapate ushindi.


Wakati huo huo, Mshindi wa droo ya 18 ya Biko ametangazwa jana, huku akiwa ni binti mwenye miaka 25 anayeishi jijini Mbeya, Linda Mhewa, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo jijini Mbeya.


Mwanafunzi huyo amepatikana katika droo iliyofanyika jana na kuchezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ikiwa ni mwendelezo wakutoka mamilioni kwa washindi wao.


Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema ni wakati wa kutajirika kwa kuhakikisha kwamba kila anayeibuka na ushindi wa Sh Milioni 20 za Biko anazitumia katika kuanzisha au kuendeleza miradi ya maendeleo kwa kupitia bahati nasibu ya Biko.


“Watu watumie vizuri uwapo wa Biko kwa kuhakikisha wanacheza mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza kuanzia Sh 1,000 na kuendelea huku Sh 1,000 ikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo droo kubwa hufanyika Jumatano na Jumapili,” Alisema.Huku mamilioni ya fedha yakiendelea kwenda kwa Watanzania, Biko wameshalipa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa mwezi Mei pekee, ikiwa ni zawadi za papo kwa hapo na ile ya droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...