https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, June 26, 2017

Tanga watakiwa kuongeza uzalishaji


 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku pichani, amewataka wananchi heri ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwataka kujiandaa na ujio wa fursa ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga kwa kuongeza uzalishaji.
 
Alhaji Mussa aliyasea hayo wakati akizungumza na mtandano huu ambapo alisema mradi huo ni mkubwa ambao utahusisha watu wengi hivyo wananchi wanapaswa kujipanga ili kuweza kuendana na fursa hiyo muhimu kwa ajili ya kujiongezea kipato halisi.
Alisema lazima wakazi wa mkoa huo watambue kuwa wakati mradi huo ni mkubwa ambao unaweza kuchangia ukuaji wa kipato chao hivyo wajiandae kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mama ntilie waweze kuendesha shughuli zao kisasa.

“Mkoa wa Tanga hasa kwenye Jimbo langu la Tanga mjini kutatekelezwa mradi mkubwa wa mradi wa boma la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hiyo wananchi wangu wajiandae kwa kuongeza uwajibika na uzalishaji ambao utakuwa na tija kwao “Alisema.
“Lakini pia niwaambie wenzetu madereva wa tax, mafundi wajiandae kikamilifu kuona namna ya kuboresha huduma zao kwani ujio wa mradi huo utalifanya Jiji la Tanga kuwa na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuweza kupata mafanikio “Alisema.
Aidha pia mbunge huyo aliwataka waumini ya dini ya kislaam kuendelea kutenda mema hata baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo kuwajali wengine.
Mbunge huyo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wana sheherekea vema sikukuu ya Iddi Salama kwa kuwa makini hasa wakati watoto wao wanapokwenda kutembelea wawe na wasaidizi.
 Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...