https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, June 18, 2017

Mkulima wa Handeni Tanga ajinyakulia Sh Milioni 20 za Biko


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMBO yamezidi kunoga katika bahati nasibu ya ‘SMS’ ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, baada ya mkulima kutoka wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, kuibuka kidedea kwa kuzoa Jumla ya Sh Milioni 20 kutoka kwenye bahati nasibu hiyo inayozidi kushika kasi nchini Tanzania, ikiwa ni droo yake ya 15 tangu kuanzishwa kwake.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania, Humud Abdulhussein kushoto, akiagana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 15 leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis aliibuka kidedea kwa kuzoa jumla ya Sh Milioni 20.

Bahati nasibu hiyo imechezeshwa leo  jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba bahati nasibu yao imezidi kupanua mbawa zake kwa kutua wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa mshindi wao Yahaya ambaye ana umri wa miaka 50 anayejishughulisha na kilimo.
Alisema ni faraja yao kuona mchezo wao umekuwa ukitoa washindi katika sehemu mbalimbali za Tanzania, akiamini kuwa ni mwendelezo wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na mamilioni ya Biko.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akichezesha droo ya 15 ya Bahati Nasibu ya Biko ambayo donge nono la Sh Milioni 20 liliangukia kwa mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis baada ya kuchezeshwa droo hiyo jana, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.
“Tunafarijika sana kuona mkulima wa Handeni Tanga naye ameibuka na mamilionin ya Biko, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kumpatia utajiri mkubwa kwa kuzitumia fedha hizi kwa umakini katika shughuli zake za ukulima, ukizingatia kuwa amepatikana kwa kucheza Biko ambao ni mchezo rahisi kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku kiasi cha kucheza kikianzia Sh 1000 na kuendelea.

Kucheza mara nyingi zaidi ndio nafasi ya ushindi, hivyo tunawaomba Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi zaidi kwa kupitia mitandao ya simu za mikononi ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo mbali na donge nono la Sh Milioni 20 linalotolewa kwa washindi Jumatano na Jumapili, pia tunatoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000 zinazolipwa kwenye simu za washindi walizotumia kuchezea bahati nasibu yetu,” Alisema Heaven.

Akizungumza kwa simu saa chache baada ya kutangazwa mshindi, Khamis, alimshukuru Mungu kwa kumletea zawadi nzuri ya Sh Milioni 20 kwa kupitia mchezo wa Biko unaochezeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa mitandao ya simu ya Tigo, Vodacom na Airtel.

“Namshukuru Mungu kwa kunipa zawadi hii kutoka Biko, nikiamini kuwa fedha hizi zitanipatia mafanikio makubwa kwa kupitia biashara zangu za kilimo ninazoshughulika nazo,” Alisema Khamis. Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdulhussein, aliupongeza mchezo wa Biko na kuongeza kuwa unachezeshwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...