https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, August 11, 2016

Mgodi wa BUZWAGI wakabidhi hundi ya sh milioni 700 Halmashauri ya mji Kahama

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi madarasa ya shule ya msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.

Na Dixo Busagaga wa Michuzi Blog, Kanda ya Kaskazini.
Mgodi wa Buzwagi umekabidhi halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo  ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.

Akizungumzia malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.

Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi.

Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma.
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Kahama wakishuhudia makabidhiano hayo.



“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata, ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”

Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
Mwisho.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...