https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, August 11, 2016

Uharibifu wa miundo mbinu ya vituo vya mabasi ya mwendo kasi ni tatizo

Fredy Njeje, Dar es Salaam
Ikiwa ni takribani miezi michache kupita tangia mabasi ya mwendo kasi yaanze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha yakiendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo vya mabasi hayo.

Hili limeonekana bila chenga Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi  vifaa vya kuhifadhia taka vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda na kulegea. 

Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa  ni ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi hiki?
Hapa upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.
Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.
Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka
Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena
Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini
Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto. 


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...