https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, July 16, 2015

Watanzania kuendelea kuula viwanja vya Bayport Vikuruti

Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavula.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATANZANIA wenye nia ya kumiliki ardhi, wataendelea kuipata fursa hiyo baada ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kuwapatia nafasi wateja wao katika mradi huo ulioanza rasmi Mei 22 mwaka huu na kuzinduliwa katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Meneja Biashara wa Taasisi hiyo, Thabit Mndeme, alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam, juu ya huduma hiyo ya viwanja vinavyotolewa kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.

Kwa mujibu wa Mndeme, wameamua kuendelea kutoa huduma hiyo ya viwanja katika eneo ya Vikuruti, baada ya kufanya tathmini kwa kuangalia umuhimu wa Watanzania kuweza kumiliki viwanja ili kujenga nyumba za kuishi, nyumba za biashara na mahitaji mengineyo wapendayo.
Mbali na huduma hiyo ya viwanja, Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa bila kusahau bima ya elimu kwa uwapendao, huku huduma zote hizo zikifanikisha maisha bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavula.

“Bayport Financial Services ni taasisi yenye kutoa huduma bora kwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, hivyo tunaamini huduma yetu ya mikopo ya viwanja kuwa endelevu ni sehemu ya kuhakikisha kwamba watu wote wanakuwa na uwezo wa kumiliki ardhi kwa ajili ya matumizi yao mbalimbali. “Hii ni huduma endelevu na muhimu inayotolewa kwa watu wote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo mteja kutoka mahali popote anaweza kumiliki kiwanja hicho kwa kuchukua fomu za kuomba viwanja hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima, bila kusahau kwa wakala wetu Bank Of Africa (BOA),” alisema.

Mndeme alisema kwamba sasa wateja wao watazidi kunufaika kununua viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku wakivipata kwa njia ya mkopo au kwa fedha taslimu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...