Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya
Kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Financial Services, jana
imewakabidhi wanafunzi wawili hundi ya Sh Milioni tatu, itakayowawezesha kila mwaka kupata Sh Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa ajili ya ada kwenye
shule zao wanazosoma kutokana na malipo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao inayoendeshwa na taasisi hiyo.
Wanafunzi
hao ni Jacqueline Ndyamkana wa shule ya sekondari ya James Sangu na Joceline
Ndyamkana wa shule ya awali, huku malipo hayo yakitokana na bima ya mama yao aliyejulikana
kwa jina la Anna Jelle, ambapo kwa kupewa kiasi hicho cha fedha kila mwaka, kutawafanya wasome bila usumbufu wowote katika kipindi hicho cha miaka mitatu mfululizo.
Alpha Akimu Meneja wa Kanda za Nyanda za juu Kusini akizungumza katika hafla hiyo. |
Shughuli ikiendelea
Watu wakiuliza maswali
Makabidhiano yakiendelea
Makabidhiano ya hundi yakiendelea
Makabidhiano yakiendelea
Asante kwa hundi
Alisema taasisi yao iliamua kuanzisha huduma hiyo ya bima ya elimu kwa uwapendao ili kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea kupata elimu zao, hata inapotokea wazazi wao wanafariki Dunia. “Ndugu yetu Anna Jelle alijiunga na huduma yao Aprili 14 mwaka jana, ambapo mwaka huu ilitokea bahati mbaya akafariki Dunia, hivyo tukaona tuwape watoto hawa stahiki zao ili waendelee na masomo yao.
“Watoto hawa watapata Sh Milioni moja kwa kila mwaka na watapewa fedha hizi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, tukiamini kuwa tunaweza kurahisha masomo yao japo kwa kipindi hiki ambacho mzazi wao hayupo,” alisema. Naye Jacqualine aliishukuru Bayport kwa kuanzisha huduma hiyo muhimu, akiamini kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo anaweza kuwa katika mazingira mazuri kwenye masomo yake na mdogo wake.
Kwa mujibu wa Ruth, malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000 na makato ya bima ya Silver ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi na kusisitiza kwamba ambapo mbali na bima, taasisi yao pia inatoa huduma ya mikopo ya bidhaa bila kusahau mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment