https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, July 16, 2015

Mbio za Uchaguzi Mkuu, Mazala aingia Singida Mjini

fomu
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoani Singida.

Na Hillary Shoo, Singida
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Singida Mjini. Akizungumza na kundi la Vijana wa CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed Dewji aliyestaafu.

kwa nguvu
Mazala akiwaasa vijana kufanya kazi kwa nguvu katika jimbo hilo.
nimenyooka
Mkinipa nafasi ya kuwatumikia mambo yatanyooka namna hii.
ninao uwezo
tuko imara
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini Hassan Philipo Mazala akisistiza jambo kwa vijana waliomsindikiza kuchukua fomu.
pamoja
vijana
Baadhi ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na Hassan Mazala nje ya jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa singida mara baada ya kuchukua fomu. Picha na Hillary Shoo

‘Nimejipima nikaona ninaweza kuvaa viatu vilivyoachwa wazi na Dewji kwani katika kipindi chote alichukuwa Mbunge nilishirikiana nae katika kuyatekeleza yale yote aliyonituma kama msaidizi wake wa karibu.” Alisema Mazala.
“Nimekuwa Kiongozi kwa muda mrefu katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye vijiji ,Kata, Wilaya, Mkoa na sasa Taifa, hivyo nina uwezo wa kutosha na nimekomaa kisiasa katika kufanya kazi hii ya Ubunge bila wasiwasi wowote pale alipoachia Dewji” Alisisitiza.
Aidha alisema anazifahamu changamoto zinazolikabili Jimbo hilo kwani ametembea kona zote na kujionea hali halisi ya wananchi wanavyojishigulisha na shughuli za kijamii.
“Nina Moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia, ninaombeni mnibebe, najua yamesemwa mengi sana juu yangu katika kipindi ambachio nimlikuwa nafanya kazi na MO, lakini yapuuzeni hayo kwani hayana ukuweli wowote ni chuki binafsi tu.” Alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana linalojiita team Mazala.
Hata hivyo Mazala ambaye ana uwezo mkubwa wa kutawa jukwaa alisema kamwe hatawaanguisha wananchi wa Jimbo hilo huku akitumia misamiati Zimwi likujualo, Usiache mbachao na mwokoto kuni porini huota moto pamoja.
Akitangaza kutogombea tena Ubunge mapema Julai 08 mwaka huu mjini Singida Dewji alimsifu Mazala kwa kusema kuwa ni mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu na ana moyo wa kujitolea kwani aliweza kusimamia kazi zake zote bila ya matatizo yoyote.
“Na pia ninapenda kumshukuru kipekee mtu mmoja ambaye bila yeye mafanikio yangu ya kiuongozi niyoyopata hapa Singida yasingeweza kufanikiwa vizuri bila ya yeye.” Alisema Dewji katika taarifa yake hivi karibuni.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...