https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, July 20, 2015

Magufuli atikisa vilivyo jimboni kwake Chato

 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .
  Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
  Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.

   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara),Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika kituo cha mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.
 Ilikuwa ni shangwe tu jioni ya leo ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli. 

   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji  wa Katoro mkoani Geita alipokuwa akipita njiani kuelekea wilayani Chato.Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli mkoani humo wananchi walijitokeza kwa wingi kila baada ya kilometa kadhaa na kuziba barabara wakita kumuona Dkt Magufuli na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake na chama cha CCM.
 Mwananchi akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dkt Jonh Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato jioni ya leo,kabla ya kumkaribisha Dkt John Magufuli aliyewasili mjini humo jioni ya leo akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na kuwashukuru.
 Dkt Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato jioni ya leo
 Dkt Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu,mara baada ya kujitambulisha kwao.
   Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.

 Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo mjini Chato mkoani Geita.

PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-GEITA

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...