https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, July 06, 2015

Kwachaga stars kuiwinda Masharika Julai 13

Na Mwandishi Wetu, Handeni
TIMU ya Soka ya Kwachaga Stars, yenye maskani yake kijiji cha Kwachaga, wilayani Handeni, mkoani Tanga, inatarajia kuingia uwanjani Julai 13, katika Uwanja wa Magamba, kukwaana na wapinzani wao Masharika, ikiwa ni michuano ya kuwania Kombe la Ng’ombe, linaloendelea kutimua vumbi. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wilayani Handeni, inafanyika siku chache baada ya Kwachaga Stars kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Kideleko.
Akizungumza mwishoni mwa wiki wilayani Handeni, Nahodha  wa timu ya Kwachaga Stars, Zakaria Nambuje, alisema kwamba vijana wake wamejipanga imara kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono dhidi ya Masharika. Alisema wamejipanga imara kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri katika mashindano hayo ya kuwania Ng’ombe, ikiwa ni michuano yenye nguvu katika maeneo ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
“Huu ni wakati mzuri wa kuwaandaa vijana wangu kwa ajili ya kuonyesha kiwango cha juu katika mashindano haya na mengineyo yatakayokuja. “Naamini kila tufanyalo kwa sasa ni kuifikiria mechi ijayo kwa sababu tunahitaji kufanya vyema na kuonyesha namna gani tumepania,” alisema.
Kwachaga ni miongoni mwa maeneo ya wilaya ya Handeni yenye vijana wengi wanaojua kucheza soka, jambo linalohitaji mipango kabambe kuhakikisha kwamba wanamichezo hao wanaendelezwaa ili waweze kupiga hatua.
No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...